📌HAMIDA RAMADHANI
MBUNGE wa Jimbo la Sengerema Tabasamu Mwagao (CCM) amesema atatumia vikao vya Bunge kulirudisha zao la Pamba katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuhamasisha usamabazaji wa mbegu za zao hilo.
Tabasamu ambaye anaingia Bungeni katika kipindi cha kwanza aliongea hayo hivi karibuni mara baada ya kuapishwa kiapo cha uaminifu katika hafla iliyofanyika Bungeni Jijini hapa.
Mimi naingia Bungeni kwa mara ya kwanza lakini nikiwa na vipaumbele vyangu, ambavyo la kwanza ni Pamba, nitahakikisha mbegu za Pamba zinasambazwa katika Mikoa ya kanda la Ziwa ili uzalishaji uongezeke.Tabasamu Mwagao
Aidha Tabasamu alisema ili zao la Pamba liweze kulimwa kwa wingi Serikali inatakiwa kuweka mfumo madhubuti katika kusambaza mbegu ambazo wakulima wengi watazipata kwa urahisi.
Kipindi cha nyuma Pamba ilikuwa ikilimwa katika Mikoa zaidi ya 16 lakini baadae pamba iliharibiwa kuanzia katika usambazaji wa mbegu, tatizolilianzia hapo.
Aidha Mbunge huyo
alisema kipaumbele chake kingine ni uboreshaji wa miundo mbinu ya maji ambapo
alisema katika jimbo lake Wananchi wake wana shida ya maji.
Vilevile Mbunge huyo
alisema akiwa Bungeni hapo atahakikisha anawasilisha tatizo la uhaba wa
madarasa ya Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Chuo cha Ufundi.
Mbunge huyo alisema
atahakikisha anatumia vikao vya Bunge hilo la 12, kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili Wananchi wa jimbo la Sengerema bila kujali itikadi zao za Vyama
au dini.
Mimi ni mtumishi wao, hivyo sitajali itikadi zao za Vyma, dini au kabila,niwatumikia Wananchi wa jimbo langu kwa usawa na kuwaletea maendeleo,nimekuja Bungeni kupiga kazi.
Mbunge huyo alisema
hata kama yeye ni wa CCM lakini hata kaa kimya kuhofia kuonekana
mbaya,linapotokea suala la kuwasemea Wananchi wake atasema kwa maslahi ya
Serikali
0 Comments