Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizindua 'Ripoti ya Utoaji wa Taarifa kwa taasisi za Umma. |
📌NA MWANDISHI WETU
AZIRI wa Habari ,Utamaduni Sanaa na
Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amesema pamoja na kuwepo kwa sheria ya Habari
,hali ya uwajibikaji wa utoaji Habari bado ipo chini katika taasisi za umma .
Dkt.Mwakyembe
amebainisha hayo leo Oktoba 2,2020 jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya
haki ya kupata taarifa duniani yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya
Habari kusini Mwa Afrika ,Tawi la Tanzania[MISA-TAN].
Dkt.Mwakyembe amesema
pamekuwepo na changamoto kwa watumishi wa umma kutokuwa na ushirikiano wa kutoa
taarifa kwa vyombo vya habari ili wananchi wajue kinachoendelea hali ambayo
husababisha wananchi hao kushindwa kupata taarifa kwa usahihi na kusababisha
malalamiko hivyo ni wajibu kwa kila mtumishi wa Umma kuwa na ushirikiano wa
utoaji wa taarifa .
Pia ,Waziri Mwakyembe
amesema kuna baadhi ya Watumishi wa umma wamekuwa hawapokei simu za waandishi
wa Habari pindi wanapohitaji taarifa muhimu hali ambayo husababisha sheria ya
haki ya kupata taarifa kuvunjwa jambo ambalo ni kinyume na maadili
ya utawala bora.
Unakuta mtumishi wa umma anapopigiwa simu na mwandishi wa habari hapokei hata simu na ukiangalia hata sababu za kutokupokea simu hazipo ni wajibu watumishi wa umma kutoa taarifa ili mwananchi ajue nini kinaendelea katika nchi yake.
Dkt.Mwakyembe
Hata hivyo,Waziri
Mwakyembe ametumia fursa hiyo kuvipongeza vyombo vya habari na wanahabari kwa
kuendelea kuelimisha jamii huku pia akipongeza taasisi za serikali
zilizotunikiwa vyeti kwa ubingwa wa utoaji wa taarifa kwa wananchi.
Aidha ,suala la
uhaba wa Maafisa habari katika halmashauri limeibuka katika maadhimisho hayo ya
siku ya kupata taarifa duniani ambapo baadhi ya wajumbe wa MISA-TAN
wametoa hoja ya kuwa na umuhimu kwa kila halmashauri kuwa na afisa habari
kuliko kuingiliana majukumu na kitengo cha TEHAMA hususan kwa wataalam wa
ICT kufanya majukumu kama wanahabari.
Akijibu hoja
hiyo,Waziri Mwakyembe amesema serikali ina mpango wa kuweka mfumo mzuri zaidi
katika kuhakikisha kila halmashauri inakuwa na Maafisa Habari.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya Habari kusini Mwa Afrika ,Tawi la
Tanzania[MISA-TAN] Bi.Salome Kitomari amesema miongoni mwa shughuli ambazo
zimekuwa zikifanywa na MISA-TAN ni pamoja na kufanya tafiti ambapo bado kuna
usiri hata mambo ya kawaida kabisa katika utoaji wa taarifa .
Utafiti ulibaini kuwa zipo ofisi za umma ambazo ukipiga simu saa za kazi haiwezi kupokelewa na wakati mwingine unaweza kudhani labda mhusika katoka kidogo.Lakini unapopiga simu mara kadhaa kwa nyakati na siku tofauti bila majibu,inatia shaka sana.
Salome Kitomari
Katika maadhimisho
hayo,shirika la Mawasiliano Tanzania[TTCL]limepata tuzo ya Uminyaji
taarifa[Golden Padlock]kutoka Taasisi ya vyombo vya Habari kusini Mwa
Afrika ,Tawi la Tanzania[MISA-TAN] .
0 Comments