📌NA HAMIDA RAMADHANI
IMEELEZWA kuwa watu bilioni 1.1 wana upungufu wa kuona huku Takribani watu milioni 253 Duniani wanakadiriwa kuwa na upungufu wa kuona wa namna moja au nyingine.
Akitoa taarifa kwa
niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi kwa vyombo vya habari
katika kuadhimisha siku ya Afya ya macho Duniani ,Mkurugenzi wa Idara ya
Tiba Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Grace
Maghembe amesema kutokana na hali hiyo ni muhimu watu kujenga desturi ya kupima
macho ili kupatiwa huduma mapema.
Amesema,Kati ya hao milioni 36 wanaulemavu wa kutokuona kabisa na asilimia 89 ya watu wenye upungufu wa kuona wanaishi katika nchi za uchumi wa chini na uchumi wa kati, ikiwemo Tanzania
Baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kutumia dawa bila kushauriwa na wataalam na kusema kuwa kitendo hicho ni hatari na vinaweza kusababisha athari kuwa kubwa zaidi kwa kutotibu tatizo husika
Amesema,watu wenye matatizo ya kuona kwa kiwango cha kati na cha juu hapa nchini wanakadiriwa kuwa ni mara tatu ya watu wasioona ambao ni takriban milioni 1.8 hivyo kwa ujumla Tanzania ina watu milioni 2.4 wenye matatizo ya kuona .
Kwa mujibu wa takwimu
hizo asilimia zaidi ya 75 ya ulemavu wa kuona wa kati na wa juu unaweza
kuepukika huku asilimia 55 ya watu wenye upungufu wa kuona wa kati na wa juu ni
wanawake.
Naye Mkurugenzi
Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambikiza Dkt James Kiologwe amesema katika
kuadhimisho siku hiyo wamejikita zaidi katika kutoa elimu ili kusaidia watu
kuchukua hatua za kujikinga kupoteza uoni wa macho.
Amesema hivi sasa
huduma za macho zimeimarika nchini ambapo huduma hizo zikiwemo za upasuaji
zomekuwa zikitolewa kwa wagonjwa.
Amesema hadi sasa watu
450 kati ya milioni moja wamefanyiwa huduma za upasuaji huku alisema lengo la
dunia ni kufanya upasuaji kwa watu 2,000 kati ya watu milioni moja kwa mwaka.
"Bado kuna kuna
changamoto kwa maana ya lengo la dunia na sisi tulipo,lakininkadri Serikali
inavyopanua huduma idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji itazidi
kuongezeka." Amesema
Kwa upande wake Rais
wa Chama cha Madaktari wa Macho Tanzania Dkt Frank Sandi alisema ziko baadhi ya
hospitali ambazo hazina madaktari wa macho hivyo kwa kushirikiana na serikali
na wadau mbalimbai ili kuona ni kwa jinsi gani kila mkoa unapata huduma za
macho
0 Comments