WANAFUNZI WAACHA SHULE NA KWENDA KUJIAJILI,KUAJILIWA KWENYE MASHAMBA YA ZABIBU

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI 

WANAFUNZI 55 katika Shule ya Msingi ya Mlangwa iliyopo Mpunguzi wameshindwa kufikia hatua ya kumaliza elimu yao ya Msingi na kukimbilia kuajiliwa na wengine kujiajiri katika mashamba ya zabibu,bustani,au kuuza zabibu na nyanya barabarani.

Kauli hiyo imetolewa jijini hapa na wanafunzi hao waliohitimu elimu hiyo ya Msingi 2020 wakati walipokuwa wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi sherehe iliyofanyika katika viwanja ya shule hiyo ya Mpunguzi

Akisoma risala hiyo mwanafunzi Estelia  Mawazo amesema wanafaunzi 55 ikiwa ni wavulana 49 na wasichana 9 wameshindwa kufikia hatua hiyo na kuamua kuajiliwa katika mashamba hayo ya zabibu huku sababu nyingine akiitaja ni pamoja na kukariria,kuhama na utoro.

" Hii ni changamoto kubwa kwani wanafunzi wamekuwa na tamaa ya maisha Hali iliyopelekea kuona elimu sio jambo la Msingi na hatimaye kuacha shule na kwenda kuajiliwa na wengine kujiajili katika mashamba ya zabibu na nyanya ," amesema Mwanafunzi Estelia.

Na kuongeza kusema"Tulianza  darasa la kwanza mwaka 2014 tukiwa jumla ya wanafunzi 204 ikiwa ni wavulana 114 na wasichana 90 lakini tuliohitimu leo ni 149 tunaiomba serikali na jamii kwa ujumla ihakikishe wanafunzi walioko shuleni wote wanamaliza na kutimiza ndoto zao," amesema Mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika mahafari hayo Faraja Maulaga muhasibu Mkuu kutoka Chuo Cha Mipango jijini Dodoma amesema maendeleo endelevu ya watoto yanaenda sambamba na utatu ikiwa ni serikali ,wajibu wa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Amesema serikali inahakikisha inatoa elimu iliyobora kwa wanafunzi wote hapa nchini,wajibu wa wanafunzi ni kusoma kwa juhudi na maharifa na jamii nikutoa malezi ili watoto wetu wawe wanafunzi Bora na nia njema siku zote.

Aidha amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na  Rais John Magufuli imeondoa vikwazo kwa walezi na wazazi katika suala zima la ada kwani ndicho kikwazo kilicho onekana wanafunzi kushinda kuendelea na kumaliza shule.

Nimesikia katika Risala yenu Wezenu 55 wameshidwa kufikia hatua hii ya siku ya Leo kutokana  na changamoto mbalimbali na hi yote ni kutokana na kujiasahau kwa wazazi na walezi katika kuwazingatia katika masomo yao watoto wetu

Faraja Maulaga.

Na kuongeza kusema " Sasa kutokana na hayo wazazi na walezi tupaze sauti zetu katika vitendo vyote vitakavyo wafanya watoto wetu wasifikie ndoto zao,tupige kelele watoto wetu wepende shule ili wasiweze kutumbukia kwenye janga kubwa la utumiaji was madawa ya kulevya,mimba za utotoni kwani Mpunguzi ya kesho, Dodoma ya kesho inatengenezwa na jamii ya Leo," amesema.

Kwa upande wa changamoto zingine amesema atazifikisha kwa Mkurugenzi wa Jiji ili ziweza kutatuliwa lakini amewaasa Wananchi watengeneze mkakati wa kuzitatua baadhi ya changamoto zinazowakabili  kutatuliwa.

"Changamoto nyingi ninazoziona hapa zipo ndani ya uwezo wetu na tunaweza wa kuzitatua hivi ni kweli tunaweza kulalamika hatuma samani za shule mbono majumbani kwetu tunazo??

Tujiwekee mkakati wa kuzitatua changamoto hizi sisi wenyewe kwa kuzipa kiaumbele na ninahakika ndani ya kipindi kifupi tutakuwa tumetatua baadhi ya changamoto na serikali ije kujaziliza vitu ambavyo nikweli hatuna uwezo navyo," amesema

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo ya Mlangwa Alfred Nyambuya nikweli watoto wanaenda kwenye biashara ndogondogo za zabibu katika eneo la njiapanda nakufanya biashara zao na wengine kuajiliwa .

Niliagaiza nitafutiwe watoto wote watoro na mwalimu Mkuu wa shule hii ya Mlangwa alinipatia majina na nikayapaeleka kwa mtendaji na mtendaji aliwashughulikia ambapo wapo waliorudi na na kuendelea na masomo na wengine kugoma kurudi shule kuendelea na masomo

Mwenyekiti wa kamati ya shule Nyambuya.

 

Ameongeza kuwa juhudi zingine kama kamati walichangishana fedha na kupata mgambo ambapo walifanikiwa kuwarejesha baadhi ya wanafunzi kwa kuwawawajibisha wazazi na Wanafunzi wenye ili waendelee na masomo

"Wapo tuliofanikiwa kuwarudisha shuleni  na kunabaadhi ya wanafunzi walikataa kurudi shule na kuendelea kufanya kazi zao za kuajikiwa na wengine kujiajili kwenye mashamba na bustan za zabibu," amesema

Hata hivyo amesema changamoto kubwa ni pamoja na  wazazi kutowasimamia watoto na kusahau kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha ya baadae ya watoto 

Pia ameeleza jitihada walizo zifanya katika kuhakikisha wanafunzi wanarudi shuleni imesaidia kupunguza utoro ambapo  apo awali utoro ulikuwa kwa Kila siku watoto 150 Mpaka 200 waliokuwa hawafiki shuleni lakini kwa ufuatioiaji kupitia mwenyekiti wa kamati ya shule hali imepungua ingawa haijaisha kabisa.

Post a Comment

0 Comments