📌NA HAMIDA RAMADHANI
WAFANYABIASHARA wadodowadogo ali maaarufu Kama Machinga waliopo Kata ya Madukani jijini Dodoma wameiomba serikali kuwapatia mikopo ili waweze kukuza mitaji yao.
Wameyasema hayo
Leo jijini hapa katika kampeni ya mlango kwa mlango duka kwa
duka mtu kwa mtu inayofanywa na Mgombea udiwani wa Kata hiyo ya Madukani
Profesa Davis Mwamfupe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Licha ya kuwa
tupo katika vikundi lakini suala zima la upatikanaji wa mikopo kwetu ili tuweze
kukuza biashara zetu imekuwa ni tatizo hivyo basi tunaiomba serikali ituangalie
na sisi wafanyabiashara wadogo na watupatie hiyo mikpo inayotolewa na Jiji
letu," amesema Mfanyabishara huyo.
Na kuongeza kusema kuwa"Sisi tunaimani kuwa serikali yetu ya awamu ya tano ni sikivu na ndio maana hata Leo tumeweza kumuona Mgombea wetu ameweza kupita kwa kila Mfanyabishara akinadi sera zake tunaomba akipita akazifanyie kazi "amesema ismail
Naye Mathew Malima Mfanyabishara wa Saa ameiomba serikali kuwapatia mikopo ili waweze kupiga hatua katika ufanyaji wao wa biashara .
Hatutaki kubaki pale pale kila siku na ndio maana tunaiomba serikali yetu sikivu itupatie mikopo na sisi wafanyabiashara ndogondogo tuweze kukuza na tuweze hata kumiliki fremu na kwakufanya hivyo tutakuwa tumekuwa na kuiingizia serikali mapato.
Mathew Malima
0 Comments