📌NA DOTTO KWILASA
TUME ya haki za Binadamu na utawala bora nchiniTanzania (THBUB) imetembelewa na viongozi kutokaTume ya haki za binadamu na utawala bora ya nchini Burundi kwa lengo kubadilishana uzoefu wa kazi .
Aidha hatua hiyo inategemewa na pande zote mbili kudumisha mahusiano bora kuhusu masuala ya utetezi wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuimarisha usalama na amani kwa nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini hapa, baada ya kutembelewa na viongozi hao Mwenyekiti wa tume hiyo nchini hapa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema ziara ya Viongozi hao wa Burundi itahusisha mazungumzo ya ujirani mwema.
Sisi na Burundi licha ya kuwa ni majirani tuna undugu pia,hivyo basi hawa viongozi wamekuja kwa lengo la kuendelea kujenga mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Burundi
Mwaimu.
Licha ya hayo Mwenyekiti huyo wa THBUB amesema ziara hiyo haihusiani na masuala ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni na kuiomba jamii kuelewa kuwa imelenga kudumisha mahusiano .
Pamoja na Mambo mengine Mwaimu amesema kama taasisi zinazoshughulikia masuala ya haki za bianadamu na utawala bora ugeni huo utakuwa na tija hasa kwa jamii inayohitaji huduma kutoka katika taasisi hizo mbili.
"Kutokana na uzoefu wa kiutendaji tunaotarajia kubadilishana Katika kikao chetu,tunatarajia kujenga uhusiano bora Katika jamii hususani kwa masuala ya haki za binadamu na uwajibikaji,"anasema .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora kutoka Burundi Dkt.Nauwimana Edourd ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt.Magufuli kwa hatua ya kuimarisha amani miongoni mwa watanzania huku akisema amani hiyo ni tunu kwa watanzania na inapaswa kuenziwa na mataifa mengine Afrika.
"Nchi yetu ya Burundi imekuwa ikishuhudia amani na mshikamano uliopo Tanzania,hakuna nasiyefahamu namna gani uongozi wa Serikali ya Tanzania inavyoendelea kutimiza haki ya kidemokrasia kwa wananchi wake,"anasema.
Amesema, kukutana na viongozi wa
tume ya haki za binadamu na utawala bora wa Tanzania hakutasaidia tu kuongeza
mahusiano mazuri ya kiutendaji baina ya Taasisi hizo mbili bali itaongeza
uhususiano mzuri baina ya nchi hizo mbili katika upatikanaji wa haki za
binadamu.
"Mara nyingi Dunia inaangalia amani Katika mtazamo wa migogoro baina ya binadamu ,lakini amani sio tu kutokuwa na vita bali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kuwa na utengamano na utulivu kwa njia ambayo watu wote duniani wataishi pamoja na kushirikiana kutatua matatizo yanapotokea,"anasisitiza Dkt.Edour.
Viongozi wengine kutoka Burundi ni pamoja na mratibu kutoka tume hiyo Nimpangaritse Inoccent , mkuu wa itifaki mbonyiyeze Paschal, na mshauri wa balozi wa Burundi kwa Tanzania Prefer Ndayishimiye.
0 Comments