📌NA DOTTO KWILASA
KADA wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Mohammed Seleman Tewa amewaomba wagombea wa nafasi mbalimbali
kufanya kampeni za kistaarabu kama zinazofanywa na Mgombea CCM,John Magufuli.
Amesema kufanya
kampeni za kistaarabu kutasababisha amani kuendelea kuwepo kwenye jamii kwani
licha ya maisha ya siasa bado Kuna maisha mengine ambayo yanategemea zaidi
amani ,usikivu na ushirikiano.
Kauli hiyo ameitoa
Jijini hapa wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na hali ya mwenendo wa kampeni
nchini,ambapo Tewa alisema Mgombea wa nafasi ya urais, John Magufuli anafanya
kampeni za kistaarabu hivyo na wagombea wa nafasi zingine za ubunge,udiwani
pamoja na urais kwa vyama vingine wanatakiwa kuiga mfano huo.
Kada huyo amesema
Magufuli amekuwa kinara wa kueleza amefanya nini na akichaguliwa tena kwa mara
nyingine atafanya nini tofauti na vyama vingine ambavyo vimekuwa vikishindwa
kutoa sera zao na kujikuta wakitoa matusi.
Wajifunze kwa Magufuli (Mgombea wa CCM) kwanza anafanya siasa za kistaarabu,anawatambulisha wabunge na madiwani kasha anaelezea atafanya nini kwa kipindi kingine,huku akieleza kwa miaka iliyopita amefanya nini
Tewa.
Vilevile amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa ni chama cha kulalamika tu na kuchezewa faulo huku kikiwa hakielezi kitafanya nini.
Kada huyo pia
amewaomba wagombea wote kutii maagizo yote yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi
(NEC) ya wanapoitwa watii maagizo kwani hao ndio wasimamizi wa uchaguzi.
Hata hivyo amesema licha ya kelele zote hizi zinazoendelea hakuna chama kinachoweza kushindana na CCM katika nafasi ya urais kwani mgombea wa CCM amefanya mambo makubwa kwa kuleta maendele ya watu pamoja na vitu.
Kuhusiana na uchaguzi
wa Zanzibar amesema utakuwa mwepesi kutokana na mgombea wa urais,Hussein Mwinyi
kukubalika kwa watu wote.
“Nawausia ndugu zangu
wa Zanzibar wasikosee kule ni Mwinyi kwani uongozi anauweza na amefanya kazi
ambazo kila mmoja anaziona,”amesema.
0 Comments