"SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA WALIMU"-JPM




📌NA HAMIDA RAMADHANI.

SERIKALI imesema  kuwa inafahamu na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na walimu na inaendelea kuwaona walimu Kama chanzo cha maendeleo hapa  nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama jijini hapa wakati akifungua kongamano la kuadhimisha siku ya mwalimu duniani lililoandaliwa na chama cha walimu Tanzania (CWT).

Maendeleo ya nchi yetu yanafungamanishwa na elimu hivyo basi ili tuweze kufikia maendeleo makubwa lazima tuipekipaumbele cha Kwanza kiwe kwenye elimu yetu ya Tanzania 

Mhagama 

Na kuongeza kusema kuwa"Lazima tukumbuke elimu ndio chachu ya maendeleo ya Taifa letu," Amesema Waziri huyo Mhagama.

Aidha wakati huo huo kabla hajafunga kongamano hilo Rais John Magufuli alipiga simu na kuongea moja kwa moja  na walimu kwa kuwapongeza kwa maadhimisho hayo.

Niwapongeze  sana walimu wenzangu leo ni siku yetu na awali ya yote kunataarifa zimekuwa zikisambaa kwamba walimu wa Cheti wanatakiwa waende wakajiendeleze sasa niwaombe  tu mzipuuze taarifa zinazoendelea kwenye mitandao kwamba walimu wenye mitaala ya cheti wafutwe narudia tena taarifa hizo mzipuuzwe niwatake tu mchape kazi

Rais Magufuli. 

Nakuongeza kusema kuwa " Kauli hizi najua ni kweli uliowazi zimesambazwa na watu wenye nia mbaya na sisi,"Amesema Rais Magufuli

Awali kabla hajamkaribisha Rais wa chama cha Walimu Tanzania CWT Leah Ulaya amesema mwalimu ndio nguzo ya Taifa katika mambo mbalimbali hivyo mwalimu anastahili kupata huduma muhimu ikiwemo na suala zima la upandwishwaji wa Madaraja. 

Hata hivyo anasema Mwalimu anaonekana kama kioo na mlezi wa jamii rai yangu jamii iendelee kuonyesha upendo wa ziada kwa walimu wote hapa nchini

Kwa upande wake Katibu Mkuu Chama cha walimu Tanzania CWT Deus Seif amesema licha ya walimu  kufanya kazi katika mazingira magumu lakini wamekuwa wakitoa elimu bora kwa wanafaunzi wao.

Aidha amesema kupitia Kongamano hilo watajadili kwa upana mafanikio na changamoto zinazowakabili Walimu wote nchini

 


Post a Comment

0 Comments