📌NA
HAMIDA RAMADHANI
MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Madukani na aliyekuwa Meya wa Jiji la Dodoma Profesa
Davis Mwamfupe ameahidi kutataua kero za umeme,ushuru na mapipa ya kuhifadhia
uchafu kwa wafanyabiashara waliopo ndani ya kata hiyo alimaarufu (one way).
akiongea na wafanyabiashara hao katika kampeni ya mlango kwa mlango Profesa Mwamfupe amesema kata ya madukani ni kata ya wafanyabiasahara hivyo lazima ahakikishe anafanya mambo makubwa ili kuhakikisha anaweka mazingira mazuri kwa wafanyabaiara wa kata hiyo.
Mambo hayo ni pamoja na mazingira mazuri ya wafanyabiashara kushushwa kwa kodi,wafanyabiashara wadogo wadogo alimaarufu (machinga) kutobughudhiwa na mtu yoyote
Mwamfupe
Aidha amesema katika suala zima la uboreshwaji wa biashara ni pamoja na kuweka taa katika eneo hilo ili wafanyabiashara wote wafanye kazi mpaka muda wa usiku au mpaka asubuhi ili wananchi wa kata hiyo na Dodoma kwa ujumla waweze kupata huduma hiyo.
Sasa hivi ukipita mida ya saa 12 hadi saa 1 usiku maduka yote haya huyakuti yakiwa wazi yote yanakuwa yamefungwa na niseme tu hatukuja hapa eti tu ni kwasababu ya kipindi cha uchaguzi bali ni jukumu letu sisi kama viongozi kuhakikisha tunawaletea maendeleo wananchi
Profesa Mwamfupe.
Awali akitoa kero mbele ya mgombea udiwani huyo moja kati ya wafanyabiashara hao Ferinanda Sibo kero zinazowakabili hapo ni pamoja na kukosa fursa za maendeleo kama vile kuomba mikopo kwa aajili ya kuendeleza biashara zao, pamoja na ushuru mkubwa.
"Juzi wamekuja hapa wametunyang'anya vichwa vya cherehani kwasababu hatujalipa ushuru na gharama ni kubwa sana sasa wanapochukua vichwa vya cherehani na kuondoka navyo sisi hiyo pesa ya ushuru tutaitafutaje hali ya kuwa vitendea kazi wamevichukua"amesema Ferinanda
Kampeni ya mlango kwa mlango bado inaendelea ambapo leo imefanywa katika
barabara ya sita,barabara ya saba na barabara ya nane lengo likiwa ni
kutaka kujua kero ya mfanyabaiashara mmoja mmoja.
0 Comments