NDEJEMBI AAHIDI MAKUBWA JIMBO LA CHAMWINO

 


📌Na Barnabas Kisengi 

Mgombea ubunge kwa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Jimbo la chamwino mkoani Dodoma Deogratus Ndejembi ameendelea na kuomba ridhaa ya wananchi wa jimbo la Chamwino kumpa ya ndiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika October  28 Mwaka huu

Akiwa katika Kata ya Msamalo kijiji cha Mgunga, Ndejembi ameendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo Wazee na wakinamama ambapo amesema wakimchagua atahakikisha anatatua shida za miundombinu ya barabara na kuongeza vyumba vya madarasa katika Kata hiyo

Najua hapa kunachangamoto ya barabara hasa kipindi cha masika na kuhakikisha wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) wanafika hapa na kurekebisha miundombinu hii ya barabara hapa.Ndejembi

Pia mgombea huyo wa CCM amesema kutokana na elimu bila malipo watoto wengi wanatarajiwa kujiandikisha kuingia shuleni hivyo atakapochaguliwa atahakikisha anaanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kukabiriana na changamoto hiyo.



Ndejembi amesema mustakabari wa maendeleo ya jimbo la Chamwino linatakiwa kuwa na kiongozi kutoka CCM hivyo amewaomba wananchi wa Kata hiyo kumpa kura za kutosha  Rais John pombe Magufuli  na mgombea udiwani wa kata hiyo ili kushirikiana kuleta maendeleo ya jimbo hilo na mkoa wa Dodoma.


Post a Comment

0 Comments