📌NA DOTTO
KWILASA
KATIKA kuendana na uchumi wa Kati, Halmashauri
ya Jiji la Dodoma imesema itaendelea kutoa habari za utekelezaji wa majukumu na
miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi kufahamu
muelekeo wa Halmashauri yao katika utoaji wa huduma bora.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha
TEHAMA na Uhusiano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa
akiongelea tukio la kihistoria la kufikisha idadi ya watu (viewers)
wanaotembelea tovuti ya Jiji kufikia 500,000.
Amesema,Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia
Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano kinawajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa habari
na taarifa kwa wananchi likiwa ni takwa la Kikatiba Ibara ya 18 (b) ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Kisheria Ibara ya 5 ya Sheria ya
Upatikanaji wa Habari ya Mwaka 2016. “Kupitia takwa hilo, tovuti ya Halmashauri
inatakiwa kutoa taswira halisi ya Halmashauri, utendaji, uwajibikaji na utoaji
wa huduma kwa wananchi.
Hivyo, tovuti ya Halmashauri ni Halmashauri
iliyorahisishwa kupitia Teknolojia ya Habari” anasema Fungo kwa msisitizo.
Fungo amesema kupitia umuhimu huo wa utoaji
habari na taarifa “idadi ya watu wanaotembelea tovuti ya Halmashauri ya Jiji la
Dodoma www.dodomacc.go.tz
"Haya ni mafanikio makubwa kwa
Halmashauri yetu. Aidha, idadi hiyo imekuwa ikiongezeka siku baada ya siku,
Leo tarehe 24 Oktoba, 2020 tunao
watembeleaji 504,993 hadi muda huu saa 11:15 watu ambao wametembelea tovuti
yetu wamefika 2,626 na wanaoendelea kutembelea sasa hivi ‘online’
63”anafafanua.
Aliongeza kuwa Mafanikio hayo ya kihistoria
yanaonesha kuwa watu wana kiu ya kupata habari na taarifa za halmashauri kila
Mara.
Idadi hii kubwa ya watu wanaotembelea tovuti yetu ni ishara kuwa wanaimani na habari na kazi nzuri inayofanywa na halmashauri yetu. Wajibu wetu ni kuendelea kutoa habari na taarifa mbalimbali zenye ubora katika tovuti ya Halmashauri ili kuwapa watembeleaji kile wanachostahili
Fungo.
Kutokana na hayo Fungo ametoa shukurani kwa
watembeleaji wote wa tovuti hiyo, menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma
na watumishi wa Jiji la Dodoma kwa michango yao na pia watumishi wote wa
kitengo anachokiongoza.
"Nawasihi watembeleaji wa tovuti hii
kuendelea kutembelea na tunatoa nafasi ya wao kushauri mambo ambayo
yatasaidia kuboresha maudhui ya tovuti hii
"Watu wanaweza kutuma maoni yao kirahisi
kwa kubofya sehemu iliyoandikwa 'Wasiliana nasi' ambayo ipo juu ukifungua
tovuti" ameshauri Fungo.
Akiongelea tofauti ya tovuti ya Jiji na tovuti
nyingine amesema ni habari zinazotolewa haraka kwa kuzingatia viwango vya
uandishi wa habari na taarifa.
“Ukiangalia wakati sisi tumepindukia
watembeleaji tovuti 500,000, Halmashauri inayotufuata inawatembeleaji chini ya
100,000 kwa upande wa Halmashauri za Majiji” alisisitiza Mkuu huyo wa Kitengo
cha TEHAMA na Uhusiano.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ujenzi katika
Halmashauri ya Jiji la Dodoma, QS Ludigija Ndatwa amesema kuwa tovuti ya Jiji
kwake ni darasa.
“Mimi ni mtembeleaji mzuri wa tovuti hiyo
karibu kila siku naitembelea,Mara nyingi huwa nataka kujua taarifa mpya za
matukio mbalimbali zilizoingia kwenye tovuti ya Jiji. Bahati nzuri huwa
nazikuta” alisema QS Ndatwa.
Kutembelea tovuti hiyo kumemsaidia kujifunza
na kufahamu mambo mengi yanayofanyika katika idara nyingine za Halmashauri
ambazo isingekuwa rahisi kuzipata kwenye vikao.
“Mfano utaratibu wa kupata kibali cha
ujenzi, mtu akiniuliza huwa sihangaiki hata kumuelezea, namwambia tembelea
tovuti ya Halmashauri utakuta utaratibu wote” amesema QS Ndatwa kwa kujiamini.
Ikumbukwe kuwa tovuti za Halmashauri
zilizinduliwa tarehe 27 Machi, 2017 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI
katika ukumbi wa Hazina, Dodoma.
0 Comments