📌NA BARNABAS KISENGI
MGOMBEA wa Udiwani wa Kata ya Kilimani jijini Dodoma Neema Mwaluko amewaomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa kata hhiyo kuhakikisha siku ya kupiga kura wanachagua wagombea wote kutoka chama hicho ili waendelee na juhudi za kuwaletea maendeleo
Akihitimisha kampeni zake katika kata hiyo Mwaluko amesema hiyo ndiyo Kata pekee ambayo wanaishi viongozi wengi wa serikali, hivyo inatakiwa iongozwe na diwani wa CCM ambaye atatatua kero mbalimbali zilizobaki katika Kata hiyo ikiwemo miundombinu ya barabara za mitaa
Neema
amesema katika mitaa nyingine ya Kilimani tayari wameshatandaza barabara za
ndani za lami hiyo watakapo
mpatia miaka mitano tena atahakikisha miundombinu ya barabara ya zilizobakia zinakamilika.
Ameongeza kuwa kwa sasa katika zoezi la upimaji lililofanyika katika mtaa wa Chinyoyo tayari wameshatenga eneo la kujenga shule ya msingi na sekondari na huduma nyingine za kijamii kwa kushirikiana na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa huo Faustina Bendera ambaye alimtengea eneo hilo la miundombinu ya ujenzi wa taasisi hizo.
Akifunga
kampeni hizo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilimani Mzee Kiwaya amewataka wananchi
kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatano 28-10-2020 na kuhakikisha wanachagua kwa mtindi wa mafiga ili iwe kata ya mfano kwa maendeleo kati ya 41 za
Jiji la Dodoma
0 Comments