CHADEMA KANDA YA KATI 'WALIA' NA TUME YA UCHAGUZI

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI  

KATIBU wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati Gwamaka Mbughi ameiomba Tume yaTaifa ya Uchaguzi NEC kurudia upya zoezi la kuwateua mawakala na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwani walioteuliwa hawana imani nao.

Hayo ameyaeleza Leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika Ofisi zao za Kanda zilizopo katika eneo la Area C jijini hapa.

" Ni ukweli usiopingika Tume ya Taifa ya Uchaguzi Imeteua wasimamizi namakalani pasipo kufanyika kwa usahilili cha ya watu kupewa fursa ya kuomba nafasi hizo za usimamizi" amesema Katibu huyo.

Na kuongeza kusema kuwa "Mfano mzuri katika Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro waneteua Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwenda kusimamia uchaguzi je kweli hapo haki itapatikana tunayo orodha ya kutosha katika majimbo yetu 29 ya wabunge ni kweli usio pingika makada wa CCM ndio wamewekwa makarani wa Uchaguzi," Amesema.

Amesema inafahamika wazi  Baada ya mchakato ya kampeni vyama vya siasa vinapewa fursa ya kuchagua mawakala watakao simama kwaniaba ya wagombea na vyama vya siasa.

Hata hivyo amesema  Tume ya Uchaguzi nayo imepewa fursa ya kuteuwa wasimamizi wasaidizi na makalani watakao simamia katika vituo mbalimbali vya kupigia kura katika maeneo yote.

Sasa wito wetu kwa tume yaTaifa ya  Uchaguzi NEC kurudia  mchakato mzima wa kuchagua wasimamizi wa saidizi mbalimbali kwani zoezi hilo halikufuata sheria na kanuni

Na kuongeza kusema Tunataka Tume itengue uteuzi na kurejesha zoezi upya katika kuwapatia makarani na wasimamizi wasaidizi wapya watakao simamia kura kwa haki katika vituo vyote vya uchaguzi Oktoba 28.

Amesema Kanda ya Kati inavituo vya uchaguzi  11,329 mpaka leo chama tumefanikisha kupata mawakala katika vituo vyote na kwamujibu wa sheria watapewa siku saba kabla ya uchaguzi kwajili ya maandalizi.

Post a Comment

1 Comments

  1. Na mimi ni mgombea wa kata ya chigongwe jimbo la Dodoma mjini kwenye kata ya chigogongwe wameteu watendaji wa mitaa yote kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye maeneo yao ya kazi.
    Sitakubali nitaleta watu wangu barabarani kukataa upuuzi huu hizi ni dalili za mwanzo kabisa za kuhujumu uchaguzi huu.

    ReplyDelete