📌NA.FAUSTINE GALAFONI
Katika kukabiliana na
changamoto ya uhaba wa vitabu vya kujifunzia katika vyuo vya kilimo hapa
nchini,Wizara ya kilimo imeamua kugawa vifaa vya
kielektroniki katika vyuo 14 vya
kilimo nchini vyenye thamani ya Tsh.Milioni 248.69.
Akizungumza na
waandishi wa Habari Agosti,31,2020 jijini Dodoma katika hafla fupi ya ugawaji
wa vifaa hivyo vya TEHAMA , Katibu mkuu Wizara ya Kilimo Gerald
Msabila Kusaya amebainisha kuwa tangu ateuliwe kuwa
katibu Mkuu wa Wizara hiyo tarehe 5,Machi mwaka huu amebahatika kufanya ziara
katika vyuo mbalimbali vya elimu ya kilimo hapa nchini na kubaini
changamoto ya uhaba wa vitabu hivyo na kuamua kununua vifaa vya kielekroniki
kwa ajili ya kujifunzia .
Baada ya kuona changamoto hiyo tulijadili na wadau tukaona namna nzuri ya kusoma kwa njia ya kielekrtoniki hivyo tumeamua kununua kununua vifaa mbalimbali hali itakayosaidia wanafunzi wetu ambao ni wataalam wa baadae wa kilimo kujifunza kwa njia ya mtandao na vifaa hivyo vikigharimu Tsh.Milioni 248.69.Gerald Msabila Kusaya
Aidha,Katibu mkuu huyo wa Wizara ya kilimo
ametoa wito kwa wakuu wa vyuo vya kilimo kuhakikisha wanasimamia vinatumika
vizuri na mara kwa mara ili kuwandaa wataam wa kilimo wanaoendana na
wakati.
Wakitoa neno la
shukrani baada ya kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya Wakuu wa vyuo 14 vya
serikali,mkuu wa chuo cha Kilimo Mlingani Samson Cheyo pamoja na kaimu mkuu wa
chuo cha Sukari (National Sugar Institute-NSI) Kilichopo Kilombero Mkoani
Morogoro Aloyce Kasmir wamesema vifaa hivyo vya TEHAMA vitarahisisha
katika ufanisi wa kujifunza.
Baadhi ya vifaa vya
TEHAMA vilivyotolewa ni pamoja na Rooter Machine,Kompyuta mpakato[laptop],Desk
top,TV vikiwa na thamani ya Tsh.Milioni 248.69.
0 Comments