📌NA HAMIDA RAMADHANI
WAZIRI Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa
anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Karibu Dodoma Festival
2020.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika viwanja vya Jamhuri Mwenyekiti wa
Tamasha hilo na msanii wa Bongo Movie Simon Mwapagata maarufu kama (Maduhu) amesema Tamasha hilo la Dodoma Festival ni Tamasha la kwanza kuandaliwa likiwa na lengo la kukuza na kutangaza mkoa na jiji la
Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuendeleza fikira za baba wa Taifa
Mwl Julius Kambarage Nyerere juu ya makao makuu pamoja na
jitihada zinazofanywa na Rais Dk John Pombe Magufuli katika kuendeleza
makao makuu ya nchi.
Tamasha la mwaka huu litakua na maudhui ya kutoa fursa Kwa makundi mbali mbali kutoa pongezi na shukrani kwa Rais Magufuli kwa kazi nzuri alioifanya kwenye makundi mbali mbali ya jamii na kwenye sekta mbali mbali ambazo zimefanya vizuri na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii
Simon Mwapagata.
Ameongeza kusema
kuwa "Tunatumia jiji la Dodoma katika kuratibu mambo makubwa
yanayounganisha taifa kwasababu Dodoma ndio makao makuu yenye kila sababu ya
kufanya mambo ya kitaifa pamoja na makundi ya sekta mbali mbali
"amesema
Aidha amesema katika
kutoa fursa iliyokusudiwa Tamasha la karibu Dodoma festival linatarajiwa
kufanyika katika siku 3 kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi
Oktoba 2020 ambapo wanatarajia Rais Magufuli kuja kufunga Tamasha hilo.
Hata hivyo amesema
makundi ya jamii pamoja na sekta mbali mbali zitapewa nafasi ya kutoa ushuhuda
kwa mabadiliko waliyo yapata Kwa kipindi cha miaka mitano cha uongozi wa
awamu ya tano.
"Haya ni baadhi
ya makundi ambayo yamepata mabadiliko ya ushindi ndani ya awamu ya Tano,Boda
boda, mama ntilie, machinga, watu wenye ulemavu, wanafunzi wa
vyuo, wanafunzi wa sekondari na msingi, vijana, wanawake, na wazee
wafungwa walio huru pamoja na waathirika wa madawa ya kulevya "amesema Mwapagata
Makundi ya sekta
mbali mbali yatakuwepo wakiwemo wavuvi, wakulima, wachimbaji wadogo,
wajasiriamali na wafanya biashara ,wasafirishaji wafugaji tour
operator wasanii wa bongo movie na bongo flava, wana michezo, na
viwanda vipya.
Sambamba na hilo Mwapagata amesema kuwa Tamasha hilo pia litahusisha shughuli mbali
mbali za kiuchumi na kijamii kama vile Burudani ya wasanii,
burudani ya michezo ,makongamano ya makundi, matembezi ya hisani na maonesho ya wajasiriamali.
0 Comments