📌NA JOYCE KASIKI
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Elim Pentekoste Peter Konki
amewataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kuombea uchaguzi Mkuu na wagombea wote hususa Rais John
Magufuli kwani ndiye Rais aliyepo
madarakani kwa sasa.
Akizungumza katika ufunguzi wa Makao makuu ya ofisi ya
Kanisa hilo yaliyopo Ihumwa jijini Dodoma Askofu Konki amesema,wagombea wote
kuanzia ngazi ya kata mpaka urais wanahitaji maombi lakini Dkt.Magufuli
anahitaji zaidi ili Mungu amlinde na kumtumza kwani mbali na kuomba kura bado
ana majukumu ya urais anayoyatekeleza.
Tunahitahi sana kumwombea Rais ,pamoja na kwamba na yeye ni mgombea ,kama utamlinganisha a wagombea wengine utakuwa umefikiri tofauti,yeye ni taa ya Tanzania na ngao yetu.
Amesema Askofu Konki na kuongeza
Tusielewane vibaya ,hakuna chama ninachokitetea ,nasimama katikati.
Amesema wakati huu wa uchaguzi ni muhimu sana waumini
kuombea wagbea na nchi kwa ujumla ili mchakato huu uishe salama na kuiacha nchi
katika hali ya utulivu na amani .
Kanisa la Elim Pentekoste lilikuwa na Makao makuu yake
mkoani Tanga lakini kutokana na ujio wa Makao Makuu mkoani Dodoma ,kanisa hilo
lilifikia uamuzi wa kuhamishia Makao makuu ya Kanisa jijini Dodoma kama sehemu
ya kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli kuhamishia Makao makuu mkoani Dodoma.
0 Comments