📌NA HAMIDA RAMADHANI
JAMII imetakiwa kuacha uoga na badala yake imeaswa
kuwatumia wasaidizi wa msaada wa kisheria hasa wanawake pale wanapo kandamizwa
kwenye suala zima la haki zao za msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana,Afisa
Ufuatiliaji Tathimini Hamisa Hamad
kutoka Pemba kwenye kikao cha
tathimini amesema lengo la kikao ni kufanya mapitio ya mambo
ambayo tumeyatelekeza ndani ya mwaka.
Katika katika kikaokazi hiki tunatekeleza mapitio tuliyoyafanya ndani ya mwaka mmoja na Kama inavyojulikana kwa sisi upande wa Zanzibar msaada wa kisheria ulikua mgeni kwetu kutokana na mila na desturi na dini.Hamisa Hamad
Anasema
Msaada wa kisheria kwa Zanzibar ilikua
ni kitu kigeni kutokana na mila na
desturi na dini lakini baada ya kufika mwaka 2007 baada ya
shirika la Legal services facility LSF)kufika ndipo wanawake 850
waliamka na kuanza kutoa taarifa za kikatili wanazo fanyiwa na wenza wao na
kupatiwa msaada wa kisheria.
"Zamani kwa sisi waafrika kwa mila zetu na
deaturi ilikua ni ngumu kutoka kwenda kumshitaki mwenza wao eti tu kwakukosea
au kwakufanyia tendo la ukatili hali iliopelekea sisi wasaidizi wa kisheria
kukosa takwimu sahihi za kuwatambua ni wanawake wangapi waliofanyiwa ukatili wa
kijinsia"amesema Msaidizi wa kisheria Hamisa
Aidha amesema
katika mila za kiafrika wanawake
na watoto ndio wanaongoza kwa kufanyiwa ukatili wa kijinsia.
MAFANIKIO.
Amesema baada ya kuja kwa wasaidizi wa msaada wa
kisheria wanawake wengi wamejitokeza na kuanza kudai haki zao za msingi ikiwemo
kudai ardhi ,asilimia 99 ya wanzanzibar ni waislam.
Amesema
katika dini ya kiislam imeainisha wazi
mwanamke akifa anatakaiwa apewe haki zake kadhaa na mwanaume haki kadhaa lakini
jambo hilo limekuwa likikiukwa na wanaume
wamekua wakiwakandamiza.
"Sasa ni vyema wanawake wote kujitokeza katika
kudai haki zao kwani mwanamke ana haki zake ya kutunzwa kupewa mirathi na
ikitokea umeachwa dai haki zako na kama ikitokea hata mwaume amefariki mwanamke
anatakiwa apewe haki zakezote "amesema Msaidizi wa kisheria Hamisa
Naye Afisa Ufuatiliaji na Tathimini kutoka mkoani
Lindi Nelson Choaji amesema kazi yao kubwa katika mkoa wa lindi ni kuhakikisha
upatikanaji wa haki katika mkoa wa Lindi unapatikana.
Hata hivyo amesema kwa upande wa Lindi Legal Service
Facility imekua ikiwapa nguvu wasaidizi wa kisheria kuhakikisha wanawafikia
watu wote wenye changamoto mbali mbali
wanazokabiliana nazo katika jamii.
Tatizo kubwa la mikoa ya pwani kesi nyingi tunazokumbana nazo ni za wanaume kutekeleza familia zao mi nitoe wito tu kwa kina mama kuwatafuta wasaidizi wa msaada wa kisheria pindi wanapo hitaji haki zao za msingi.Nelson Choaji
Legal Service Facility ni Shirika lisilo la kiserikali
lenye makao Makao Makuu yake jijini Dar es salaam lengo kuu la uanzishwaji wake
ni kusaidia jamii kupata haki.
0 Comments