NA.FAUSTINE GIMU
GALAFONI
Katibu mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya jamii,,jinsia ,Wazee na Watoto Prof.Mabula Nchembe amewataka
waganga wa tiba asili hapa nchini kuzingatia sera,kanuni na taratibu za Afya
huku akiwataka kuacha kutumia vifaa ambavyo hawakupata mafunzo rasmi
na ufanisi wake .
Prof.Nchembe
amebainisha hayo jijini Dodoma katika maadhimisho ya miaka 18 siku ya tiba
asili ya Mwafrika ambapo pia amehimiza Waganga wa tiba asili
kuachana na matangazo yasiyofaa na kuweka mabango ovyo ovyo barabarani .
Hivyo waganga tiba asili ni vyema tukazingatia sera, taratibu ,sheria na kanuni za Wizara ya afya,hususan katika suala la uwekaji mabango ovyovyo barabara na kuweka matangazo yasiyofaa ,pia matangazo ya tiba asili katika vyombo vya habari lazima yapate kibali kutoka Baraza la Tiba Asili na tiba Mbadala.Prof.Mabula Nchembe
Baadhi ya wadau wa tiba za Asili na tiba
Mbadala wakiwa katika maadhimisho ya miaka 18 ya tiba asili ya Mwafrika
yaliyofanyika kitaifa viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Aidha,Prof.Nchembe
amewahimiza watoa huduma wa tiba asili na tiba mbadala nchini kuhakikisha kuwa
wamesajiliwa wao wenyewe,wasaidizi wao,vituo vyao vya kutolea
huduma na dawa zote zinazotumika.
Hali
kadhalika,Prof.Nchembe amebainisha kuwa tangu mwaka 2017 serikali
ianze kusajili dawa za asili kupitia Baraza la Tiba Asili
na Tiba Mbadala hadi sasa dawa thelathini(30)zimesajiliwa.
Kuhusu kuadhimisha
miaka 18 ya siku ya Tiba Asili ya Mwafrika,Prof.Nchembe amesema
Tanzania imefanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambua huduma ya tiba
asili katika sera ya afya kuanzia mwaka 1990 na kama ilivyohuishwa mwaka 2007,
kutungwa kwa sheria ya tiba asili na tiba
mbadala Na.23 ya mwaka 2002 ,Tanzania kuwa miongoni
mwa nchi 46 za Afrika zinazoadhimisha siku hii kuanzia mwaka 2003.
Mambo mengine ni
pamoja na kuundwa kwa baraza la Tiba Asili na tiba
Mbadala mwaka 2005 ,kutengenezwa kwa miongozo na kanuni mbalimbali
za tiba asili na tiba Mbadala mwaka 2005-2010 pamoja na kuanzishwa
kwa mifumo rasmi ya kiutendaji ndani ya serikali.
Kaimu msajili wa
Baraza la Tiba Asili Patrick Seme amesema baraza hilo limekuwa
mstari wa mbele kusajili katika kuwasajili waganga wa tiba asili ili
watambulike kisheria hali ambayo husaidia kuondoa watoa huduma wa
tiba asili wasio kuwa waaminifu.
Kwa upande wake Kaimu
Mkuu Idara ya utafiti wa tiba asili iliyo chini ya Taasisi ya ya
Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt. Vitus Nyigo amesema wakati wa
janga la Corona walifanya tafiti za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo
mchanganyiko wa tiba lishe zikiwemo limau,tangawizi,pilipili,vitunguu maji na
vitunguu vya kawaida .
Kaulimbiu ya
Maadhimisho ya 18 tiba Asili ya Mwafrika ni “Miongo Miwili ya Tiba Asili Afrika 2001-2020
nchi zina mafanikio gani” ambapo kauli mbiu hiyo
inakumbusha kujitathmini tiba asili ilikotoka hadi ilipo na namna
bora ya kuboresha .
0 Comments