📌NA HAMIDA RAMADHANI
UMOJA wa Wagaga na Wakunga wa Tiba
Asili Tanzania (UWAWATA) wameiomba Serikali kupunguza gharama za upimaji wa
sampuli za dawa pindi zipelekwapo kwa mkemia mkuu.
Akizungumza na waandishi wa Habari
kwenye banda lao katika Viwanja vya Nyerere Square kwenye wiki ya Tiba
Asili Afrika Mwenyekiti wa Bodi za dawa za asili
kutoka UWAWATA Nurdin Lyimo amesema kiwango cha kupima dawa ni kikubwa na
gharama nyingi wanatumia mpaka kupima kutokana na wengi wao kutoka mikoani
kwenda Dar es salaam .
Tunatoka mikoani tukifika pale kupima dawa ni zaidi ya laki 6 hapo na bado utatumia gharama nyingine za nyumba za kulala wageni bado hujala na unatumia zaidi ya siku mbili tatu kwahiyo mi niiombe tu Serikali kwakweli itupunguzie gharama hiziNurdin Lyimo
"Siyo wote wanaweza kumudu
gharama hiyo kuna wengine wana dawa nzuri kabisa lakini bei ni kubwa
wanashindwa hivi juzi tulikumbwa na janga la ugonjwa wa Corona sisi
tukatengeneza dawa inayoitwa NUT inayotibu ugonjwa huo lakini mchakato
haukuwa mrefu nadhani lilienda haraka kutokana na uzito wa ugonja lakini kiukweli
mchakato ulikua mrefu" amesema
Naye Mratibu wa Mafunzo ya kuinua
Tiba asili nchini Ally Maganyari ameiomba serikali isambaze Maabara za
upimaji wa sampuli za dawa katika kila mkoa ili kuweza kupunguza msongomano.
Niiombe tu serikali yetu chini ya uongozi wa Rais wetu Jonh Magufuli itusogezee hizi maabara kwa sababu na yeye pia amesharuhusu sisi tufanye kazi basi tunaomba na hili pia atusaidie.Ally Maganyari
Pia ameitaka jamii isiwe na imani
potofu ya kuwa waganga ni wachawi na badala wajikite katika kuamini kwamba dawa
za asili ni zinatokana na mimea ambayo inaota katika ardhi ya Tanzania.
"Tiba asili siyo uganga wala
uchawi zamani enzi za mababu zetu wamekuwa wakitumia tiba asili na wanaonekana
kuwa na maisha marefu na miili yenye nguvu siyo sawa na karne hii, hakuna kitu
kilichoumbwa na Mungu halafu kikawa kibaya kwenye asili hakuna madhara,"amesema
Hata hivyo Maadhimisho ya siku ya
Tiba Asili ya mwafrika yalianza rasmi mwaka 2003 baada ya mawaziri wa afya wa
nchi wanachama wa shirika la afya duniani kanda kuridhia kuwepo kwa
sherehe hizo.
0 Comments