📌NA HAMIDA RAMADHANI
IMEBAINIKA kwamba
Vyama vingi vya Siasa vinawatumia wanawake katika shughuli za uhamasishaji
katika kuongea idadi ya wanachama na kueneza Sera za chama ikiwemo
wakati wa kampeni katika kuwavuta wapiga kura lakini haimuoni mwanamke
kama mdau kwa ajili ya nafasi ya uongozi.
Pamoja na changamoto hizo sote tumekuwa tukishuhudia namna ambavyo wanawake kadhaa ambao walipata fursa ya kuongoza waliweza kuongoza kwa ustad na weledi mkubwa wakati mwingine kuliko hata wanaume
Alhad Salumu.
Ameongeza kuwa hayo yote na mengine mengi wanawake ni watu wenye nguvu na uwezo katika uongozi hivyo wapewe nafasi kwa kuwachagua kwaajili ya maendeleo ya taifa tukiamini wazi wataendeleza vita ya rushwa,ufisadi,dawa za kulevya, na mengine mengi kwa ustawi wa taifa ikiwemo kusimamia haki za wanyonge.
Amesema kamati ya amani inaamini kwamba wanawake akichaguliwa katika nafasi ya uongozi atakuwa na fursa ya kutunga sera na kushiriki katika vyombo vya maamuzi ambapo maendeleo na mapinduzi makubwa katika taifa la Tanzania yatatokea.
"Ikumbukwe kwamba wanawake ni zaidi ya nusu ya idadi ya wanawake duniani hivyo ili kutokomeza umasikini ni lazima wanawake wapewe nafasi na kushirikishwa kikamilifu katika uongozi sasa nafasi imefika mwanamke achaguliwe na kuwekwa mbele kwani tunaamini atafanya mambo mengi na kwa ufanisi zaidi" amesema Alhad Salumu
Pia ametoa wito wao kama viongozi wa dini na viongozi wa amani ni kuona vyama vya siasa na watanzania wote Kwa ujumla wanahitaji kuchagua viongozi walio bora ikiwemo wanawake kwaajili ya maslahi mapana ya taifa kwa vizazi vya sasa na vitakavyokuja.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake (TAMWA)Rose Ruben amesema ushiriki wa wanawake katika siasa na katika ngazi ya maamuzi ni eneo lililo na changamoto lukuki na hivyo inahitaji kuhimizwa na uongozi wa ngazi za juu, asasi za kiraia, wanawake wenyewe na viongozi wa dini.
Takwimu zinaonesha kwamba ni asilimia 37 tu ya wanawake ndio waliopo katika ngazi za maaumuzi bunge lilopita, hata hivyo bado tunaona kuna mapengo katika ushiriki wao ambayo hayana budi kuzibwa
Rose Ruben
Ameongeza kusema kuwa " Mapengo hayo ni pamoja na lugha zalilishi wakati wa uchaguzi zinazowakatisha tamaa wanawake kuwania nafasi za uongozi, uteuzi usiozingatia jinsia katika ngazi ya siasa hofu na kutojiamini kwa wanawake wenye nia ya kugombea na ilani za vyama visivyozingatia jinsia "amesema Rose
Aidha amesema mapengo mengine yaliyobainika ni pamoja na rushwa ya ngono yanatotajwa kutumika katika uchaguzi, rushwa ya kifedha, uchumi duni kwa wanawake wanaotaka kugombea na hivyo kupelekea kushindwa kufanya kampeni, mila na desturi kandamizi zinazowazuia wanawake kushiriki katika kampeni.
Amesema TAMWA inawasihi viongozi wa dini kuendelea kuhimiza wanawake kushiriki katika siasa na ngazi za maamuzi kwani wanaaminika Katika jamii.
"Viongozi wa dini mna nafasi kubwa katika jamii kuondoa mila na mitazamo potofu inayochochea ushiriki duni wa mwanamke katika siasa na katika ngazi ya maamuzi, na pia wanatakiwa wahubiri amani na mshikamano katika kipindi cha uchaguzi na amani hiyo itapatikana iwapo makundi yote maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu na mshikamano watashiriki kikamilifu katika uchaguzi "amesema Rose
MKUU WA WILAYA YA DODOMA
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga akimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuhakikisha wanadumisha aman utulivu na umoja hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu 2020.
Amesema kumekuwepo na muamko mkubwa kwa wanawake kuwania nafasi mbali mbali za uongozi Toka 2015 lakini kwa mwaka 2020 idadi ya wanawake imeongezeka zaidi tena wenye sifa.
Wanawake sasa wamekua wajasiri na wengi wameonesha wana uwezo wa kufanya kazi kubwa tena iliyotukuka
Josephat Maganga .
0 Comments