📌NA PENDO MANGALA
KITUO cha taarifa kwa wananchi(TCIB) kimeaanda
muongozo wa kuwasaidia Wabunge katika kusimamia maamuzi mbalimbali yanayofanywa
na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya umma.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Meneja
mradi wa kituo hicho,John Kitoka mara baada ya kutoa mafunzo kwa wadau
mbalimbali wa masuala ya manunuzi kuhusiana na masuala ya manunuzi na
Mikataba ya Umma.
Kitoka amesema kuwa hiyo ni kutokana na utafiti mdogo waliofanya na kubaini kuwa wabunge wengi kutojua taratibu na kanuni na Sheria za usimamizi wa manunuzi ya umma hivyo itawasaidia kuwaongezea maarifa katika kuisimamia Serikali Pamoja na kuihoji juu ya miradi mbalimbali inayoitekeleza.
Muongozo huu utawasaidia waheshimiwa wabunge kuwafumbua macho na kuweza kuihoji Serikali namna mbalimbali wanavyotekeleza miradi ya umma kwani wao ndio wawakilishi wa wanachi hivyo ni vizuri wananchi wakawa wanajua masuala ya maendeleo yanavyofanyika.John Kitoka
Aidha amesema kuwa pia muongozo huo
utawasaidia Wabunge kuhakikisha manunuzi ya umma yanafanyika kwa kufuata
taratibu za kisheria na miradi inatekelezwa kwakuzingatia sheria za manunuzi na
michakato yote inayopelekea upatikanaji wa miradi na michakato na utekelezaji
wake inazingatia misingi ya uwazi na wajibikaji.
Kwa upande wake Annex Moza ambaye ni
Afisa Miradi wa TCIB,amesema kuwa Muongozo huo utawasaidia
kuangalia kwa jinsi gani wabunge wanaweza kuisaidia serikali kutimiza
majukumu yake katika kufanya manunuzi.
Sisi kama kituo cha taarifa kwa wanachi tunaamini kwa muongozo huu tutaweza kuwapa Wabunge mbinu zaidi katika kuisimamia Serikali katika suala zima la bajeti ili kuleta maendeo na ufanisi
Annex Moza
Katika hatua nyingine amegusia suala la Mikataba mibovu ambapo amesema ni suala sugu katika nchi za kiafrika na hiyo ni kutokana na mifumo iliyopo ikiwepo usiri na hivyo kusababisha kuwepo kwa mikataba hiyo mibovu isiyotekelezeka na kuisababishia Serikali hasara.
Daniel Msangya ni mmoja wa baadhi ya
wadau waliopata mafunzo kuhusiana na Mikataba ya manunuzi Serikalini , amesema
manunuzi yanachukua sehemu kubwa ya fedha za Serikali
hivyo ni lazima kuwepo mifumo ya wazi na imara ili kudhibiti
upotevu wa fedha nyingi za umma na Mikataba ya manunuzi lazima ifanywe kwa
uwazi.
Awali akiwasilisha mada Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Tarifa kwa Wananchi (TCIB), Deus Kibamba amesema kuwa Manunuzi ya serikali yanahitaji kufanyika katika uwazi kuanzia hatua za mwanzoni kabisa kwenye kuandaa mradi, kutangaza tenda ,kutoa tenda kwa wazabuni na hata utekelezaji wa mradi ili wananchi kuwa na uelewa juu ya miradi inayotekelezwa .
Tanzania inapambana kutatua tatizo hilo ili miradi ikamilike kwa wakati, ufanisi na ubora uendane na thamani ya pesa ya mradi husika
Deus Kibamba.
0 Comments