TAKUKURU YAKANA KUBAMBAKIA WANANCHI KESI ZA RUSHWA,UTAKATISHAJI FEDHA


📌NA HAMIDA RAMADHANI 

TAASISI ya Kuzuia na kupambana  na Rushwa  TAKUKURU imekanusha taarifa zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba taasisi hiyo na serikali  imekuwa ikiwabambikia wananchi kesi za tuhuma za Rushwa na Utakatishaji wa Fedha na baadaye kutaifisha fedha za watuhumiwa hao kutoka katika akaunti  zao za Benki.

Akiongea  na Waandishi wa habari jijini Dodoma,Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU  Brigedia Jenerali John Mbungo amesema  taarifa hizo sio za kweli na ni taarifa zenye nia ovu ya kujenga chuki dhidi ya wananchi na serikali yao. 

Tunapenda kuujulisha umma wa Watanzania utambue kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa  na Dkt John Magufuli inafanya kazi yake kwa  weledi mkubwa na kwamba suala kama hili halijawahi kutokea.

Brigedia Jenerali Mbungo. 

Na kuongea kusema kuwa "Wananchi wa Tanzania wanalindwa na katiba ya Nchi na ndio maana wanapotuhumiwa kwa makosa yoyote yakiwemo ya Rushwa watuhumiwa hao huwa na haki ya kujitetea ikiwa nipamoja na kuwa na Mawakili, ".Amesema. 

Aidha amesema wananchi wafahamu  kuwa Takukuru inapokuwa imepokea tuhuma, inafanya kazi ili ushahidi dhidi ya tuhuma  hiyo.

Mara baada ya kukamilisha upatikanaji wa ushahidi huo, jalada la uchunguzi linapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP) kwa ajili ya mapitio ya ushahidi tuliokusanya

Na kuongeza kwamba "DPP akiridhika na ushahidi ulio kwenye kwenye jalada la uchunguzi ndipo kesi inafunguliwa mahakamani," amesema. 

Hata  hiyo Brigedia Jenerali Mbungo amewataka wananchi watambue kwamba watu ambao  wamekuwa wakizotoa tuhuma  hizo za kwamba Takukuru au Serikali kwa ujumla inawabambikia wananchi kesi sio kweli na wanania ovu .

Alitoa Rai kwa watanzania wasikubali kudanganywa na maelezo rahisi ya aina hiyo na wapuuze  taarifa zote za aina hiyo zinazotolewa na baadhi ya watu wasio wazalendo kwa taifa. 

Amesema Taasisi ya kuzuia  na kupambana  na Rushwa ambayo ndio chombo kilichopewa dhamana ya kuongoza mapambano dhidi ya Rushwa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia  na kupambana na rushwa Na. 11 ya mwaka 2007,inatekeleza majukumu yake Kwa kuzingatia sheria, Haki na weledi mkubwa. 

KUELEKE UCHAGUZI MKUU.

 Aidha amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu wa viongozi taasisi hiyo imekua ikijielekeza zaidi katika kueleimisha na kuhabarisha Umma  dhidi ya athari za rushwa katika uchaguzi,  umuhimu wa kuchagua kiongozi muadilifu na mzalendo, umuhimu wa kutorubuniwa na mtu yoyote na hatimaye kushindwa kutumia haki yake ya kuchagua kiongozi sahihi. 

Amesema wanafanya hivyo kwa kutambua kuwa kuelimisha jamii ni moja ya majukumu ya msingi ya chombo hicho kilichopewa dhamana ya kuongoza mapambano ya rushwa hapa nchini. 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa inapenda kusisitiza kuwa sheria na kanuni za uchaguzi mkuu wa nwaka 2020 zitumike kikamilifu kwa lengo la kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki

Brigedia Jenerali Mbungo

 


Post a Comment

0 Comments