SERIKALI imesema kuwa
makusanyo ya fedha yameongezeka kutoka Bilioni 688.7 kwa mwaka wa fedha 2015/2016
hadi kufikia trilioni2 na bilioni 699 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 hiyo ni
kutokana na kuwepo kwa mifumo ya ukusanyaji maduhuli kwa njia ya kielektroniki.
Hayo yameelezwa leo
Sept 16,2020 Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango,Dotto James wakati wa mawasilisho ya utafiti wa GePG inavyotumika
katika Taasisi za Serikali uliofanywa na wataalam toka Chuo Kikuu cha
Dar-es-Salaam.
James amesema kuwa
kuwepo kwa matumizi ya mifumo hiyo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maduhuli
katika Taasisi za Serikali imeleta mafanikio makubwa katika uongozi wa Rais
Magufuli ikiwa ni pamoja na kusaidia kuondoa mianya ya wizi,kuwepo kwa uwazi
na uwajibikaji kwa watumishi.
Hata hivyo amewataka
maafisa masuhuli ambao wanasimamaia miradi yenye misamaha ya kodi kuwasilisha
taarifa za misamaha ya kodi VAT kupitia mifumo hiyo ya kielektoniki.
Awali akiwasilisha
utafiti huo wa matumizi ya mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya
kielektroniki GePG,Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam,Profesa
Joel Matebe amesema kuwa utafiti huo ambao ulikuwa unapima tathmini
umefanyika katika Taasisi za Serikali 306 na Mikoa 11 imeonyesha
kuongezeka kwa maduhuli Pamoja na uaminifu huku akiitaka Serikali kuwaondolea
changamoto za kiutendaji kwa watendaji wa mifumo hiyo.
Nao baadhi ya
watumiaji wa huduma hizo akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi
ya jamiiNSSF)William Erio amebainisha mafaniko yaliyopatikana tangu waanze
kutumia mfumo huo mwaka 2018huku Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa bima ya Afya
nchini NHIF,Alexander Sanga amesema mfumo huo umeongeza uwajibikaji
pamoja na uwazi.
GePG ni Mfumo wa
kielektroniki unaowezesha ukusanyaji wa fedha za umma kielektroniki ambao
umebuniwa na kutengenezwa na wataalamu wa ndani wa Serikali.
Aidha na upo
kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma (Public Finance Act, 2001) ya mwaka 2001
kupitia marekebisho ya mwaka 2017 (Sura 348), na Waraka wa HAZINA Namba 3 wa
mwaka 2017 huku Mfumo huu ulianza kutumika rasmi mnamo tarehe 01 Julai 2017
ambapo ulianza na taasisi saba (7)Kwa sasa Mfumo huu unatumiwa na taasisi za
Umma 668.
0 Comments