📌NA DOTTO
KWILASA.
SERIKALI
kupitia Wizara ya fedha na Mipango imepokea jumla ya shilingi bilioni
32.9 ikiwa ni gawio kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania.
Kati ya
fedha hizo, shilingi bilioni 18.99 ni gawio huku bilioni 14 ikitolewa na
kampuni hiyo Kama sehemu ya zawadi yake katika kuchangia
shughuli za maendeleo.
Akipokea Gawio hilo kutoka kwa Airtel
Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya fedha na mipango, Dotto James amesema kiasi
hicho cha gawio kitasaidia katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo
ya nchi.
Amesema katika historia ya uwekezaji wa
serikali katika kampuni zenye uwekezaji wa hisa chache kiasi hicho hakijawahi
kufikiwa na mwekezaji yeyote huku akiongeza kwamba bodi na menejimenti ya
Airtel Tanzania iendelee kufanya kazi kwa bidi ii kuepuka kuingia hasara kama
ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya
Wakurugenzi wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Gabriel Malata mesema kuwa hivi sasa
ubia baina ya Serikali na Kampuni hiyo umeimarika ambapo serikali inamiliki
hisa asilimia 49huku airtel ikimiliki hisa asilima 51.
Aidha amesema hisa hizo zimeongezeka kutoka
asilimia 40 na kwamba hayo ni mafanikio makubwa kwa Serikali na hivyo kwa sasa
Serikali kupitia msajili wa hazina itakuwa inapata gawio la bilioni18.99 kwa
mwaka.
Hata hivyo amesema kuwa utekelezaji huo
umeenda sambamba kuhakikisha wabia wanapata gawio kama walivyokubaliana ikiwa
ni pamoja na kutoa mchango wa bilioni 14 kama mchango wa maendeleo.
Pia kampuni hiyo imekuwa ikijihusisha katika huduma mbalimbali za kijamii na katika kukabiliana na virusi vya corona iliweza kuchangia kiasi cha Sh milioni 700 .
Mwenyekiti huyo amesema ili kuhakikisha
malengo hayashuki ni lazima watahakikisha wanaiboresha aitel Tanzania kuwa na
huduma bora zaidi ikiwa ni pamoja na kuwa na siku maalum ya airtel pamoja na
kufanya tathmini nchi nzima wanapotoka,walipo na wanapokwenda.
Naye Msajili wa Hazina Athumani Mbuttuka
amesema kuwa katika Kupitia utendaji na umiliki wa kampuni ambayo serikali ina
hisa,katika kipindi cha miaka miwili iliyopita serikali imefanikiwa kuongeza
umiliki wake katika kampuni za Airtel kutoka asilimia 40 hadi 49.
Kampuni zingine ni pamoja na Udart kutoka asilimia 49 hadi 85,Keko pharmaceuticals limited asilimia 40 hadi 70,na Mecco kutoka asilimia 2 hadi 25.
Athumani Mbuttuka
Aidha amesema kuwa uchambuzi bado unaendelea
katika kampuni nyingine kama Inflight Catering Services Limited.
"Napenda kuwaasa bodi na menejimenti ya
Airtel kutoridhika na gawio mlilolitoa kwa serikali na wanahisa
wengine bali muendelee kudhibiti matumizi huku mkiimarisha teknolojia katika
utoaji wa huduma na kuhakikisha kuwa kampuni hairudi tena ilikotoka ambako
kumezaa makubaliano haya tunayoyatekeleza"amesema.
0 Comments