📌NA HAMIDA RAMADHANI
TAASISI isiyo ya kiserikali ya Organisation for Social Support Initiative and Environment Conservation (OSSIEC) imetoa msaada wa chakula na mtaji wa biashara kwa mama Sara Ulanga mwenye mtoto albino anayeishi katika kata ya Chang'ombe alietelekezwa na mzazi mwenzie mara baada ya kujifungua mtoto mwenye ualbino.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo mara baada ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi kutoka OSSIEC Kennedy Kasian amesema wao kama taasisi wameguswa kumtembelea na kutoa msaada kwa mama huyo baada ya kupewa taarifa ya mazingira anayoishi mama huyo na mtoto.
Hii ni mara ya pili, tulikuja awali na ni kweli tumeona mama huyu anapitia wakati mgumu hasa katika suala zima la kumhudumia mtoto katika afya, chakula mavazi na malazi ndipo tukaona kuna jambo tunaweza kufanya kwa mama huyu ndio maana leo tupo hapa"amesema Kasian
Watu wenye ualibino mara nyingi hufariki kwa saratani ya ngozi hivyo inahitajika juhudi kubwa kuhakikisha wanapatiwa kofia, mafuta, nguo, miwani na chakula.
Kennedy Kassian
Aidha ametoa wito kwa jamii kuacha kuwatenga wazazi na watoto wenye ualibino kwani wanaume wengi wamekuwa wakiwakimbia watoto wenye ualibino huku wakiwaita kuwa ni watoto wa laana.
Sambamba na hayo Mkurugenzi Kassian ametoa rai kwa asasi zote za kiraia kuendelea kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu.
Hata hivyo ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kupigana na kuhakikisha maisha ya watu wenye ualibino yanakuwa salama.
Sasa hivi ni kipindi cha uchaguzi lakini hali ni shwari hatujasikia wala kuona matukio yoyote yanayowahusu ndugu zetu albino hii yote ni jitihada ya serikali kuhakikisha wanaweka salama maisha ya watu wenye ualbino.Kennedy Kassian
Naye afisa utawala kutoka OSSIEC Farida Msuya amesema ulemavu siyo ugonjwa na wala hauambukizi hivyo watu wenye ualbino wanatakiwa kulindwa na kupendwa kama watu wengine.
Kwa upande wake mama mwenye mtoto huyo Sara Ulanga ameishukuru taasisi ya OSSIEC kwa msaada huo kwani maisha yake ni magumu na yakubahatisha hasa katika zoezi la kumlea mtoto huyo.
Mimi baada ya kujifungua mtoto huyu nilitengwa na kila mtu marafiki zangu, ndugu,na hata mzazi mwenzangu niliezaa nae alinikimbia mpaka aliwahi kudiliki kusema nimtupe mtoto huyu chooni kwa maana hana uhakika kama mtoto huyo ni damu yake kwakua hakuwahi kufikiria kama atapata mtoto mwenye ualibino
Sara Ulanga
OSSIEC ni shirika lisilo la
kiserikali liloanzishwa june 2020 ikiwa imejikita kwenye
Elimu, afya, Mazingira, na kusaidia watu wenye mazingira magumu.
0 Comments