📌NA
DOTTO KWILASA.
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC ) imewatoa hofu wapiga kura wenye mahitaji
maalumu kuwa maelekezo yametolewa kwa watendaji wa uchaguzi kutoa kipaumbele
kwa watu wenye ulemavu,wajawazito,akina mama wanaonyonyesha waliokwenda na
watoto vituoni,wazee na pamoja na wagonjwa.
Wito
huo umetolewa jana jijini hapa na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji
Mstaafu Mbarouk S.Mbarouk wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa
Dodoma ambao umehusisha viongozi wa dini,wawakilishi wa vijana , wanawake,wenye
ulemavu na wazee wa kimila.
Akitoa
ufafanuzi ,Makamu mwenyekiti huyo ameeleza kuwa, kwa watu wenye ulemavu wa
kuona ,kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na kifaa cha maandishi ya nukta
nundu (Tictile Ballot Folder) hiyo ni kwa wale wanafahamu kutumia
maandishi hayo na kwa wasioweza wataruhusiwa kwenda kituoni na mtu anayemwamini
wakuweza kumsaidia.
Kwa
mujibu wa Jaji Mstaafu huyo amesema hatua imefikiwa baada ya Tume kupata idadi
ya watu wenye ulemavu waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu
ambapo kuna jumla ya watu 13,211 wenye ulemavu na kati yao wenye ulemavu wa
macho ni 2223,4911 wana ulemavu wa mikono na 6077 wana ulemavu wa aina
nyingine.
Wenye ulemavu wa kuona kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na kifaa cha maandishi ya nukta nundu hiyo ni kwa wale wanafahamu kutumia maandishi hayo na kwa wasioweza wataruhusiwa kwenda kituoni na mtu anayemwamini wakuweza kumsaidia
Jaji Mstaafu Mbarouk S.Mbarouk
Hata
hivyo, Jaji Mbarouk amesema kwa wenye ulemavu wa viungo vituturi (viboksi vya
kupigia kura) vitakavyotumika kupigia kura vinaruhusu kuwahudumia kwani kuna
pande mbili tofauti ambapo upande mmoja kuna urefu wa kutosha na kikigeuzwa
kinakuwa kifupi kumuwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.
Katika hatua
nyingine NEC imevitaka Vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali za
uongozi ikiwemo Urais,Ubunge na Udiwani kuzingatia maadili ya uchaguzi katika
kipindi cha kampeni zao ikiwa ni pamoja na kuepuka lugha za kashfa
,maneno ya uchochezi ambayo yatatishia amani ya nchi.
Makamu mwenyekiti huyo
amesema,ikiwa maadili yatazingatiwa itasaidia kuepusha malalamiko kwa
jamii na kwamba haki itasaidia kuiweka Tanzania salama kimataifa na kuchochea
uchumi.
Kama kutakuwa na malalamiko yoyote basi hatua stahiki zichukuliwe ikwemo kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili ndani ya muda uliowekwa na si vinginevyo.
Jaji Mstaafu Mbarouk S.Mbarouk
Aidha amesema Tume
inaendelea kusimamia na kuendesha uchaguzi kwa kutumia sheria za uchaguzi hivyo
vyama vya siasa,wagombe na wananchi wanakumbushwa kuwa katika kipindi
hiki sheria nyingine za nchi hazijasimama hivyo wanapaswa kujihadhari na
vitendo ama matamshi ambayo kusababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi.
‘’Tume inawahakikishia
wananchi kuwa imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata
katiba sheria,kanuni na miongozo mbalimbali na kuwa kila mdau akitimiza wajibu
wake kwa kufuata taratibu watanzania wataweza kupiga kura kwa amani siku ya
uchaguzi’’anasema
![]() |
Makamu Mwenyekiti wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu
Mbarouk S.Mbarouk,akiwa katika picha za pamoja na baadhi ya Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.
0 Comments