NEC YAPITIA RUFAA ZA WAGOMBEA UBUNGE,UDIWANI NA YAFANYI MAAMUZI


📌NA DOTTO KWILASA
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)katika kikao chake cha  juzi  imepitia, imechambua na kuzifanyia uamuzi rufaa za wagombea Ubunge na Udiwani zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa Wasimamizi mbalimbali wa Uchaguzi nchi nzima. 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi  Dkt.Wilson Mahera alisema Rufaa hizo zimewasilishwa chini ya kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa Ubunge na Udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa.. 
Dkt.Mahera aamesema chini ya kanuni ya 32 (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, ikisomwa pamoja na kanuni ya 30 (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2020, Tume inaweza kukubali au kukataa rufaa hizo’’
Pamoja na hayo ameeleza kuwa Katika kikao hicho, Tume imezipitia, kuchambua na  imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 67, kati ya hizo rufaa 5 ni za Wagombea Ubunge na 62 ni za Wagombea Udiwani. 
Kwa upande wa rufaa za wagombea Ubunge, Tume imekubali rufaa tatu(3) za wagombea ambao uteuzi wao ulitenguliwa hivyo wagombea hao wanarejeshwa katika orodha ya wagombea. 
Rufaa hizo ni kutoka kwenye majimbo ya Igalula na Tunduru Kusini. 
Vilevile, Tume imekataa rufaa mbili za wagombea ambao hawakuteuliwa,rufaa hizo ni kutoka kwenye majimbo ya Ludewa na Meatu. 
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa  Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 62 za Madiwani na imekubali rufaa 29 na kuwarejesha wagombea Udiwani katika orodha ya wagombea Udiwani. 
Amezitaja rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Isalauanu (Mafinga Mjini), Nakapanya (Tunduru Kaskazini), Vijibweni (Kigamboni), NghongÊ»onha (Dodoma Mjini), Ilala (Iringa Mjini), Ilala (Iringa Mjini), Kamagambo (Kagera), Makole (Dodoma Mjini), Uhamaka (Singida Mjini) na  Bigwa (Morogoro Mjini).

Nyingine ni pamoja na Bereko (Kondoa), Majengo (Tanga Mjini), Mzenga (Kisarawe), Nangano (Liwale), Isange (Busekelo), Mburahati (Ubungo), llolo (Songwe),Kimara (Ubungo), Chang'ombe (Dodoma Mjini), Kakukuru (Ukerewe), Ruaha (Iringa Mjini) na Ruaha (Iringa Mjini). 
Pamoja na kata hizo nyingine ni Hombolo bwawani (Dodoma mjini), Nakapanya (Tunduru kakazini), Vijibweni (Kigamboni), Hazina (Dodoma Mjini), Nalasi Mashariki (Tunduru Kusini), Mburahati (Ubungo) na Mbasa (Kilombero)’’alisema.

Licha ya hayo ameeleza kuwa tume hiyo imekataa rufaa 23 za wagombea Udiwani ambao hawakuteuliwa. 
Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Kisaki (Singida Mjini), Mbati (Tunduru), Mnadani (Dodoma Mjini), Uru Mashariki (Moshi Vijijini), Ayasanda (Babati), Itiji (Mbeya), Dareda (Babati Vijijini), Mwansanze (Tanga Mjini), Endamaghang (Karatu), Kalulu (Tunduru Kaskazini), Uyole (Mbeya Mjini).

Nyingine ni  Mwananyamala (Kinondoni), Mbulumbulu (Karatu), Mhango (Bariadi), Nkangamo (Momba), Mlimani (Handeni Mjini), Mughanga (Singida Mjini), Kalembo (Ileje), Chang'ombe (Dodoma Mjini), Ikana (Momba), Malezi (Handeni), Itubukilo (Bariadi) na Mwamaumatondo (Bariadi). 
Vilevile imekataa rufaa 10 za kupinga wagombea Udiwani walioteuliwa. 
Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Bunju (Kawe), Kibeta (Bukoba Mjini), Bugogwa (Ilemela), Wambi (Mafinga Mjini), Gibishi (Bariadi), Ilomba (Mbeya Mjini), Mnyeu (Newala Vijijini), Kamsamba (Momba), Usambara (Bumbuli) na Ubungo (Ubungo). 
Mahera amesema idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa uamuzi na Tume kufikia 153 na za wagombea Udiwani 393 na kwamba Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume. 

Post a Comment

0 Comments