📌NA BARNABAS KISENGI
CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma
kimezindua kampeni za kuwania nafasi ya ubunge na madiwani kupitia tiketi ya
chama hicho katika Kata ya Dabalo.Jimbo la Chamwino wilayani Chamwino.
Akizindua kampeni Mjumbe wa
kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mgombea wa jimbo la Kongwa
mkoani Dodoma Job Ndugai amewataka madiwani wa mkoa wa Dodoma
kuondokana na fikra za kupata fursa za kuvuna fedha huku wakisahau kuwatumikia
wananchi waliowapigia kura.
Ndugai amesema baadhi ya wateule wa nafasi ya
Udiwani fikra zao wamezielekeza kwenye halmashauri kwa ajili ya kupata posho
Madiwani wengi wenu mmekuwa mnatafuta nafasi hizo kwa kujinufaisha nyinyi binafsi na kuwaza posho za vikao tu badala ya kuwatumikia wananchi kutatua kero zao katikaJob Ndugai
Wakimnadi mgombea Ubunge wa jimbo
hilo la Chamwino,wagombea kutoka majimbo mengine ya mkoa wa Dodoma akiwemo
mgombea wa jimbo la Mvumi Livingston Lusinde na George Simbachawene wamesema
mgombea wa CCM Deogratus Ndejembi anatosha kwa Jimbo la Chamwino.
Pia wamewaomba wananchi hao kuwapatia kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dkt.John
Magufuli, pamoja na madiwani wa CCM ili waweze kuleta maendeleo katika Jimbo la
Chamwino ambalo ndipo inapopatikana Ikulu.
Rais Magufuli ameleta heshima kubwa mkoani Dodoma hivyo hatuna cha kumlipa zaidi ya kumpa kura nyingi za heshima
George Simbachawene
Hata hivyo Simbachawene amewasihi
wananchi wa Chamwino kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 28 Oktoba ili kutumia
haki yao ya kikatiba ya kuchagua.
Mgombea huyo wa jimbo la Kibakwe
amewaambia wanaCCM kwamba kitakachotoa ushindi kwa madiwani,wabunge na Rais ni
kura zao tu.
Msiseme tu Magufuli atashinda,Deo Ndejembi atashinda,kama hamtoenda kupiga kura huo ushindi haupo.George Simbachawene
Kwa upande wake mgombea wa jimbo
hilo Deogratus Ndejembi amewaomba wananchi wamwamini kwamba yeye ni mtu
sahihi katika kutatua kero za jimbo hilo na atahakikisha 10% za vijana,
walemavu na wanawake zinatengwa katika halmashauri ya Chamwino na zinawafikia walengwa.
SOMA HII PIA:MAVUNDE:MITANO ILIYOPITA NILIKUWA NAJIFUNZA NIPENI MITANO TENA NIFANYE MAAJABU
SOMA HII PIA:MAVUNDE:MITANO ILIYOPITA NILIKUWA NAJIFUNZA NIPENI MITANO TENA NIFANYE MAAJABU
0 Comments