📌NA BARNABAS KISENGI
MGOMBEA ubunge Jimbo la Chamwino
mkoani Dodoma Deogratus Ndejembi kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
ameanza kampeni ya kuomba kura za Rais, Mbunge na Madiwani kwa mikutano ya kata kwa kata, kijiji kwa kijiji na kitongoji kwa kitongoji katika Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma.
Mgombea huyo ambaye alikuwa Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa ameanza kampeni
yakeya kijiji kwa kijiji kwa kukutana na makundi maalum ya wajasaliamali
wakiwemo bodaboda na mamalishe katika Kata ya Haneti kijiji cha Izava na Segeli
.
Nimeanza kukutana na makundi haya ndiyo yanajumuisha watu wengi na pia wanachangamoto nyingi hivyo ni lazima nikutane nao na kuweka mikakati ya kuwainua kiuchumi na kutatua changamoto zinazowakabili kwa kipindi cha miaka mitano (5) watakachonichagua.
Deogratus Ndejembi
Pia Ndejembi amesema kama wananchi
watamchagua kuwa mbunge atahakikisha Jimbo hilo linakuwa la mfano kwa maendeleo
katika mkoa wa Dodoma.
Mgombea huyo amefafanua kwamba
kutokana na uwepo wa makazi ya Rais wa Tanzania jimboni hapo panahitaji mtu
mwenye uwezo kusukuma maendeleo kuendana na kasi ya maendeleo katika eneo hilo
na mkoa wa Dodoma.
Ziara hiyo ateendelea nayo kwa
kuhakikisha anaongea na makundi yotekatika Jimbo hilo lenye Kata kumi na 14 za
Jimbo hilo la chamwino
0 Comments