Kaimu Mkurugenzi wa Tiba,Wizara ya afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia , Wazee na watoto Sarah Maongezi |
📌NA DOTTO KWILASA
JUMLA ya watu 1000 huzaliwa na
ugonjwa wa Sikoseli kila siku duniani huku nchini Tanzania watu 11 Elfu
wanakadiriwa kuzaliwa na ugonjwa huo kila mwaka.
Hayo yameelezwa jijini hapa na Kaimu
Mkurugenzi wa Tiba,Wizara ya afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na watoto
Sarah Maongezi wakati akizindua mwezi wa kuelimisha jamii juu ya ugonjwa wa
Sikoseli .
Aidha maadhimisho hayo ambayo huanza
kila mwaka ifikapo Septemba 1 hadi 9 yana lengo la kupeana uelewa wa
Sikoseli kati ya wadau wa afya na jamii kwa ujumla.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa
Tanzania ni nchi ya tano duniani kuwa na idadi ya wagonjwa wengi wa Sikoseli
huku ikishika nafasi ya nne barani Afrika.
Nchi zenye wangonjwa wengi duniani
ni Nigeria,India,Kongo,Angola na Tanzania,ambapo kwa Afrika Tanzania inashika
nafasi ya nne hali inayopaswa kutiliwa mkazo zaidi kuhakikisha ugonjwa huu
unazuiwa.
Sarah Maongezi
Licha ya hayo alisema ,nchini
Tanzania ,kila watoto 100 wanaozaliwa nchini ,8 kati yao wana ugonjwa wa
Sikoseli.
Ameongeza kuwa,licha ya juhudi
nyingi zinazofanywa na wizara ya Afya katika kuelekeza nguvu za uelimishaji
jamii juu ya ugonjwa huo ,jamii bado haina uelewa wa kutosha hali
inayosababisha unyanyapaa kwa waathirika wa ugonjwa huo.
Kutokana na hayo daktari bingwa wa
magonjwa ya damu kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa Stella Malangahe alisema
ugonjwa huo husababisha athari mbalimbali ikiwemo ini,figo,mapafu,kupooza na
hata vifo vya mapema.
Amesema kuwa mtu mwenye ugonjwa wa
selimundo huongezewa damu marakwa mara kwasababu chembechembe zao haziwezi
kukaa muda mrefu.
Kukiwa na mgonjwa wa Sikoseli basi lazima mama au baba yake ana ugonjwa huo.
Stella Malangahe
Akizungumzia dalili za ugonjwa huo
Dr.Malangahe amesema kuwa ni pamoja na maumivu ya mara kwa mara yanayojirudia,
kuvimba miguu,mikono na hasa mtoto anapokuwa ametimiza miezi 6,kulia Sana na
kupata manjano mikononi na miguuni,kupungukiwa damu mara kwa Mara.
Licha ya ugonjwa huo kuonekana ni
tishio,Dr.Malangahe amesema kwa sasa unatibika na kwamba mgonjwa anatakiwa
kuwekewa uboho wa ndugu wa karibu ambaye hana historia ya ugonjwa huo.
Ugonjwa wa Sikoseli unazuilika ,nawashauri wenza kabla ya kuingia kwenye mahusiano wanapaswa kufanya vipomo vya kubaini vinasaba vya ugonjwa huo ili kuzuia kupata watoto wenye Sikoseli.Stella Malangahe
0 Comments