MFUMUKO WA BEI WABAKI PALEPALE




📌NA HAMIDA RAMADHANI

SERIKALI imesema mfumuko  wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti mwaka huu umebaki kuwa asilimia 3.3 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai mwaka huu.

Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti mwaka huu kuwa sawa na mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai mwaka huukumechangiwa na kupungua na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Agosti mwaka huu zikilinganishwa na bei za mwezi Agosti mwaka jana.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Sensa za Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja amesema hii inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia agosti mwaka huu imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi julai mwaka huu.

Kwa mfano baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi agosti nwaka huu zikilinganishwa na bei za mwezi agosti mwaka jana ni pamoja na mahindi kwa asilimia 5.8,unga wa ngano kwa asilimia 1.1,mihogo kwa asilimia 16.3 na viazi vitamu kwa asilimia 11.9

Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula ziliongezeka bei kwa mwezi agosti mwaka huu zikilinganishwa na bei za mwezi agosti mwaka jana ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.2,ada za skuli za msingi na sekondari za binafsi kwa asilimia 2.4 na huduma za malazi kwenye nyumba za wageni kwa asilimia 2.8
Ruth Minja 

Amesema  mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi agosti mwaka huu umepungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.8 kwa mwaka ulioishia mwezi julai mwaka huu.

Huku hali ya mfumuko wa bei kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi agosti mwaka huu ikiwa ni Nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi agosti mwaka huu umebaki kuwa asilimia 4.36 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi julai mwaka huu.

Kwa upande wa Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi agosti mwaka huu umepungua kidogo hadi asilimia 4.6 kutoka asilimia 4.7 kwa mwaka ulioishia mwezi julai mwaka huu
Ruth Minja 

Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi Nchini.

Post a Comment

0 Comments