📌NA PENDO MANGALA
WIZARA ya Fedha na Mipango imezindua mpango wa Mkuu
wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia 2019/2020
hadi 2029/2030 ambao umelenga kuongeza wigo na fursa za upatikanaji
wa huduma za fedha kwa wananchi wote zikiwemo za bima.
Akizindua mpango huo leo Sept.17,2020 jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dotto James,Naibu Katibu Mkuu Mary Maganga amesema mpango huo utaongeza wigo katika upatikanaji wa huduma za mikopo ,akiba ,uwekezaji na kuongeza mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa uchumi unaoendeshwa na sekta ya viwanda.
Amesema,mpango huo umeandaliwa ili utumike kama
nyenzo ya kutatua changamoto zilizopo ambapo pamoja na mambo mengine
pia umelenga kuongeza upatikanaji mitaji ya muda mrefu, upatikanaji
huduma jumuishi za fedha na kulinda watumiaji wa huduma za fedha .
Pia amebainisha kuwa mpango huo wa miaka 10 unalenga kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha ,kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika sekta ya fedha ,kudhibiti utakatishaji fedha haramu na kuweka mazingira wezeshi ya sheria ,kanuni ,taratibu na miongozo katika sekta ya fedha.
Kwa upande wa vyuo vikuu na taasisi za utafiti
amewataka kuona fursa zilizopo katika mpango huo na kujipanga katika kuboreshan
maeneo mbalimbali ya kitaaluma na kiutafiti ili kuhakikisa sekta hiyo
inaendelea kuwa yenye ushindani na kuweza kuhimili mabadiliko ya nyakati kwa
wepesi na weledi.
Akitoa maelezo ya mpango huo, Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Dkt.Charles Mwamwaja amesema wakati wa maandalizi,timu ya wataalam wa Mpango huo ilifanya mapitio kwenye nyaraka mbalimbali zikiwemo taarifa za maboresho ya sekta ya fedha ,Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025,Dira ya Taifa ya Maendeleo Zanzibar ya mwaka 2020 na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza umasikini Zanzibar (ZSGRP III) .
Pia Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/17-2020/21 na taarifa ya Programu ya Tathimini ya Sekta ya Fedha yam waka 2018 kwa lengo la kupata matokeo zaidi katika utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa.
0 Comments