MISA TAN YAWANOA WALIMU WA SHERIA ZA HABARI





TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika –MISA TAN imeendesha mafunzo ya siku tatu(3) jijini Dodoma ili ‘kuwanoa’ walimu wa masomo ya sheria za habari kutoka vyuo mbalimbali nchini.

Akizungumza baada ya mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki,Mjumbe wa Bodi ya MISA TAN,Michael Gwimile amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wahadhiri na wakufunzi wa masomo hayo ili waweze kuendana na mabadiliko ya sheria katika tasnia ya habari.


Gwimile amesema mabadiliko yanayofanyika katika tasnia hiyo yamewalazimu MISA TAN kuona umuhimu wa ‘kunoa’ kundi hilo ili waweze kutayarisha waandishi mahiri kwa ustawi wa taifa.

Misa Tan kushirikiana na Internews  tunaamini kama kundi hili muhimu litakuwa na uwezo wa kufundisha wanafunzi,tutapunguza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo Waandishi katika mambo ya sheria
Gwimile


Mjumbe huyo wa Bodi ameongeza kuwa mafunzo hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga msingi mzuri wa kutatua changamoto zilizopo kwenye mitaala ya masomo ya sheria za habari.

Kwa upande wao wakufunzi waliodhuria mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yamekuwa fursa kubwa kwao ikiwemo kubadilishana uzoefu.

Licha ya kubadilishana uzoefu,wakufunzi hao wanasema wamepata maarifa mapya kutoka kwa wasilisha mada yatakayowasaidia kuandaa waandishi mahiri watakaolisaidia taifa siku za usoni

Nimepata muda wa kuzijua sharia mbalimbali zinazoendesha vyombo vya habari,pia nimeona kuna haja ya kubadilisha mitaala yetu ili kuendana na mabadiliko ya sharia yanayofanywa mara kwa mara ndani ya tasnia ya habari
Aneth Chuma Mhadhiri Msaidizi kutoka Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCO)


Naye Manning Yusuph Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Kikuu Huria (Open University of Tanzania,amesema mafunzo yamemuongezea mbinu mpya za ufundishaji.

Mhadhiri huyo amesema uwepo wa Wawasilisha mada wazoefu wakiwemo waandishi wakongwe kwenye tasnia kumempa uwanja mpana wa kufundisha huku akitumia mifano hai.
Uzoefu nilioupata umeeongezaa kitu,nimepata mifano ya changamoto ambazo waandishi wamekuwa wakikumbana nazo zitokanazo na sheria za habari.
Manning Yusuph.


Wakili James Marenga akiwasilisha mada

Katika semina hiyo Mwanahabari na Wakili James Marenga aliwasilisha mada kuhusu sheria mbalimbali za habari ikiwema Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.

Mwanahabari mkongwe Abubakar Famau ambaye pia ni ‘ripota’ wa BBC nchini,alitoa uzoefu kuhusu sheria za habari kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Senegal,Uganda na Libya ambako alishawahi kufanya kazi za habari 

Post a Comment

0 Comments