📌 DW SWAHILI
UMOJA wa Mataifa watimiza miaka 75 wakati ukiwepo ukosefu wa wazi wa mshikamano miongoni mwa nchi zenye nguvu duniani
Umoja wa Mataifa siku
ya Jumatatu tarehe 21.09.2020 inaadhimisha miaka 75 ya kuasisiwa kwake wakati
dunia ikiwa katika janga kubwa la kiafya la virusi vya Corona ambalo
limeionesha wazi hali tete iliyopo ya ushirikiano wa kimataifa.
Kumbukumbu hiyo itafungua rasmi mwanzo wa vikao vya kila mwaka vya baraza kuu ya Umoja wa Mataifa ambapo kawaida viongozi na wajumbe kutoka takriban nchi 200 wanakutana pamoja kujadili kuhusu matatizo ya dunia na kutoa mapendekezo ya ufumbuzi.
Hata hivyo mwaka huu
hali itakuwa tofauti eneo la Manhattan halitoshuhudia hekaheka ya misafara
isiyokuwa na mwisho ya magari ya kifakhari ya washiriki wa mkutano huo
mkuu,wala waandishi habari na wakalimani kwenye kumbi za Umoja wa Mataifa.
Badala yake kutokana
na Covid-19 bado kuzuia duniani kote shughuli za watu kusafiri, kila nchi kati
ya nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa 193 itaruhusiwa kutuma muwakilishi
mmoja na ambaye tu tayari yuko Marekani. Wengine wote wanahitajika kushiriki
mkutano huo kupitia njia ya vidio ikiwemo kiasi ya viongozi 160 hadi 170 wa
nchi na serikali wanaopanga kuhutubia mkutano huo.
VIONGOZI WA NCHI WATAKAOHUTUBIA
Rais wa Urusi Vladmir
Putin anajiandaa kuhutubia mkutano huo kwa njia ya vidio siku ya Jumanne na
rais wa China Xi Jinping ambaye katika kipindi cha nyuma wamekuwa
wakiwaacha wanadiplomasia wao wa ngazi za kuu kuzungumza kwenye mkutano huo kwa
niaba yao pamoja na rais Donald Trump.
Na siku ya Jumatano
utakuwa uwanja wa rais wa Venezuela Nicolas Maduri ambaye sehemu kubwa ya dunia
inamuoana kama kiongozi asiyekuwa halali. Lakini kwa upande mwingine viongozi
ambao hawana mpango wa kuzungumza mbele ya hadhara kuu hiyo ya Umoja wa Mataifa
ni pamoja na rais wa Syria Bashar al Assad na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim
Jong Un. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumzia juu ya
hilo amesema kwamba suala la diplomasia kufanya kazi linahitaji yawepo
mawasiliano na ni masikitiko kwamba wameshindwa kupata fursa ya kuwaleta pamoja
viongozi wa mataifa yote.
Kadhalika kiongozi
huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amebaini kwamba itakuwepo mikutano mingi kwa njia
ya mtandao ya pembeni mwa mkutano huo wa baraza kuu ambayo itajadili masuala
kadhaa ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi,migogoro ya Libya na Lebanon miongoni
mwa mwasuala mengine.
Azimio la maadhimisho
Maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa inasherehekewa kwa kutolewa pia azimio la pamoja lililotawaliwa na nia njema pamoja na mwito wa kupambana na ubinafsi.
Hata hivyo sura hiyo
inatofautiana na ukweli wa mambo ulioshuhudiwa tangu uripuke ugonjwa wa
Covid-19 mwanzoni mwa mwaka huu ambako imeshuhudiwa mipaka
ikifungwa,ushirikiano ukipungua na nchi zikilazimika kila mmoja kuwa na msimamo
wake. Bertrand Badie profesa kutoka taasisi ya mafunzo ya siasa ya Paris
anasema nchi zenye nguvu zilipoteza fursa ya janga la virusi vya Corona
kuimarisha ushirikiano wa kidunia.
Na badala yake
ushirikiano ulivunjika vipande vipande kutokana na madai kwamba China na
shirika la afya duniani WHO zilichukua hatua za mwendo wa kobe kushughulikia
mripuko huo. Na Marekani nayo ikatangaza itasimama kivyake na kujiondowa katika
shirika hilo la WHO.
Badie anasema matukio hayo yameonesha ni kwa
jinsi gani nchi zenye nguvu zimesababisha kushindwa hata kwa baraza la usalama
la Umoja wa Mataifa ambalo kimsinghi liliundwa kuongoza pale inapotokea
changamoto kubwa kama hii ya kuitetemesha dunia.
0 Comments