📌NA NOEL STIVIN
MGOMBEA Udiwani kata ya Mlembule kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mpwapwa Wilson Mgunga amefariki dunia.
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wilaya ya Mpwapwa Jackson Shilluah amesema Mgombea huyo amefariki usiku wa kuamkia tarehe 02 Septemba 2020 katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma (General) alipokuwa akipatiwa matibabu .
Shilluah amesema Mgunga alikuwa diwani wa kata ya Mlumbule kwa awamu mbili mfululizo na aliteuliwa na CCM na kupitishwa na Tume ya Uchaguzi kugombea awamu ya tatu katika uchaguzi wa mwaka huu.
Taarifa kamili ya chanzo cha kifo chake waganga (Daktari) wake wanaweza wakawa nazo ila tunajua chanzo cha kuanza kuugua ambapo alipata ajali ya pikipiki ambapo Mgunga akiendesha pikipiki aligonga gari aina ya Noah na alivunjika miguu, mkono pamoja na mbavu tatu.Jackson Shilluah
Msimamizi wa wa uchaguzi wa wilaya ya Mpwapwa Sweya Mamba amesema kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinataka kusitishwa kwa uchaguzi katika eneo hilo ambalo mgombea aliyepitishwa amefariki na utafanyika ndani ya siku 30 baada ya uchaguzi.
Aidha Bwana Sweya amesema tayari ameshatuma taarifa hizo Tume ya Uchaguzi na kuwataarifu vyama vyote kusitisha kwa zoezi la Kampeni katika kata hiyo kwa nafasi ya udiwani na hadi hapo Tume itakapo toa maelekezo mengine.
0 Comments