📌NA.FAUSTINE GIMU GALAFONI
MGOMBEA Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM)Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewaomba wananchi kumpa kura ili aweze kuongoza tena
kwa kipindi cha miaka mitano (5) mingine kwani miaka mitano iliyokwisha alikuwa
anajifunza .
Mavunde amesema hayo katika mkutano wa Kampeni
uliokuwa unafanyika kata ya Ihumwa jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa endapo
atachaguliwa kuwa kiongozi atafanya maajabu katika jimbo hilo.
Nataka niwahakikishie DUWASA 2020/2021 wamepanga bajeti kuhakikisha maji yanasambaa katika eneo lote la kata ya Ihumwa,miaka mitano niliyokuwa naongoza nilikuwa najifunza vile.Anthony Mavunde
Aidha,Mavunde amesema amesema suala la
barabara atahakikisha wanakamilisha katika kata hiyo endapo atachaguliwa tena.
Barabara Mhe.Rais aliahidi barabara tunahakikisha mkituchagua tena tunakamilisha ,pia umeme tutahakikisha unaenea maeneo yote 34 yaliyobakiAnthony Mavunde
0 Comments