📌NA MWANDISHI WETU
UJENZI wa Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma umekamilika kwa asilimia 87 baada ya Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuzielekeza takribani Sh. bilioni 2.3 zilizotolewa na Kampuni ya Bharti Airtel ya India kujenga Hospitali hiyo.
UJENZI wa Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma umekamilika kwa asilimia 87 baada ya Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuzielekeza takribani Sh. bilioni 2.3 zilizotolewa na Kampuni ya Bharti Airtel ya India kujenga Hospitali hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Mhandisi wa Ujenzi wa jengo la Hospitali ya Uhuru, Bw. Girimu
Kanansi, wakati Afisa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando,
alipotembelea hospitali hiyo kuangalia maendeleo ya ujenzi wake, Mkoani Dodoma
Bw.
Kanansi amesema kuwa jengo hilo lililokamilika kwa asilimia 87 linajengwa kwa
weledi mkubwa na Kampuni ya Suma JKT kupitia vijana wazalendo wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT), kinyume na awali ambapo majengo makubwa kama hayo yalikuwa
yanajengwa na kusimamiwa na wageni kutoka nje ya nchi.
Kazi inayoendelea ni kutengeneza sakafu, kuweka mifumo ya umeme na kuskimu kuta, hivyo ninaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel kuona umuhimu wa kupeleka huduma za Afya karibu na wananchi.
Mhandisi
Kanansi.
Amesema
kuwa Jengo hilo lilitarajiwa kukamilika mwezi mei mwaka huu, lakini
ilishindikana kutokana na changamoto ya msimu wa mvua kali ambao ulisababisha
kutokuwa na mazingira rafiki ya kusafirisha vifaa kwenda eneo la ujenzi.
Aidha
kutokana na hali hiyo Mkandarasi aliomba kuongezewa muda, ambapo anatarajia
kukamilisha ujenzi Oktoba mwaka huu iwapo hakutakuwa na changamoto yeyote
itakayojitokeza ikiwemo ya kutofika kwa vifaa vya ujenzi kwa wakati.
Kwa
upande wake Afisa Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Jackson Mbando, amesema kuwa kampuni
yake imekuwa na utaratibu wa kutembelea eneo hilo la ujenzi ili kuona maendeleo
yake kwa kuwa ni sehemu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo
hususani miradi ya Afya ikiwemo Hospitali ya Uhuru ambayo kupitia Mbia mwenza
Bharti Airtel ya Tanzania ndio iliyotoa kiasi cha Sh. bilioni 2.3 kwa Serikali
ambayo ilizielekeza katika ujenzi wa hospitali.
Amesema
Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kutambua uhitaji wa huduma ya Mawasiliano,
tayari imefungua maduka manne Wilayani Chamwino likiwemo eneo la Hospitali ya
Uhuru ambayo yataendelea kutoa huduma ikizingatiwa kuwa baadaya ya hospitali
kuanza kufanya kazi huduma za fedha zitahitajika.
Akizungumza
na waandishi wa Habari wakati wa Kampuni ya Airtel Tanzania ikitoa Gawio kwa
Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James alisema
kuwa, Serikali ya Tanzania ilianza uchunguzi wa umiriki wa Airtel Tanzania na
baadae kufanya mazungumzo na Kampuni mama ya Bharti Airtel ya India kuanzia
mwaka 2018 na kufanikisha Serikali kumiliki asilimia 49 ya hisa za kampuni
hiyo.
Alisema
makubaliano hayo yaliyosababisha kunufaika kwa pande hizo mbili ndiyo
yalimfanya Mwenyekiti wa Bharti Airtel ya India, Bw. Sunil Mittal kutoa Sh.
bilioni 2.3 kwa Serikali ikiwa ni shukrani kwa kuanza makubaliano mapya yenye
tija.
Katibu
Mkuu Bw. Doto James, alisema kuwa Serikali iliona vema fedha hizo zipelekwe
kujenga hospitali ya Uhuru Mkoani Dodoma ambayo inatarajiwa kumalizika mwezi
Oktoba mwaka huu.
0 Comments