📌NA. FAUSTINE GIMU
GALAFONI
Katibu mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony
Sanga ametoa rai kwa taasisi zote nchini kuhakikisha zinakuwa na Mpango
kabambe wa kutenga bajeti ili kuwawezesha wahitimu wa vyuo vikuu wa fani
ya uhandisi kujishikiza katika taasisi hizo Mara tu wanapohitimu kabla ya
kupata ajira kuliko kuzurura mtaani.
Mhandisi Sanga amebainisha hayo Septemba
4,2020 jijini Dodoma katika akifunga mkutano Mkuu wa 17 wa Mwaka wa
Wahandisi uliokwenda na kaulimbiu isemayo;
"Katika
mapinduzi ya 4 ya Viwanda vipi uelekeo katika kukabiliana na changamoto
za dunia"
Katika kutoa motisha na kuwapa moyo vijana kuipenda fani ya uhandisi ni lazima kuangalia mbinu pindi wanapohitimu wasiwe wa kuzurura njia sahihi ni kuwaandalia mazingira hivyo ni vyema taasisi kuaandaa bajeti ya kuwawezesha kujishikiza katika taasisi hizo kabla ya kuajiriwa kuliko kuwaacha wanazurura mtaani kwani fani ya uhandisi ni nyeti mno kwa maendeleo ya taifa.Mhandisi Anthony Sanga
Aidha,ametumia fursa hiyo kuwakumbusha
wahandisi waliokula kiapo cha uaminifu kuhakikisha wanazingatia maadili
ya taaluma yao .
Pia Mhandisi Sanga amewapongeza Wahandisi kote
nchini kwa kufanikisha Tanzania kuivusha katika uchumi wa kati na kubainisha
kuwa uwezo waliojengewa Wahandisi katika mkutano huo utakuwa chachu kwa
maendeleo ya Taifa.
Kuhusu ufuatiliaji,Mhandisi Sanga ameitaka
bodi ya Usajili ya Wahandisi kuhakikisha inafuatilia kwa makini na muafaka
maazimio kwa ajili ya kufanya mrejesho baadae .
Mwenyekiti wa bodj ya Usajili ya Wahandisi Mhandisi Prof .Ninatubu Lema amesema karibu washiriki 3500 wameshiriki mkutano huo wa Mwaka wakiwamo washiriki 500 waliokuwa wakifuatilia kwa njia ya mtandao kutoka maeneo tofauti ya dunia.
Mwenyekiti wa bodj ya Usajili ya Wahandisi Mhandisi Prof .Ninatubu Lema amesema karibu washiriki 3500 wameshiriki mkutano huo wa Mwaka wakiwamo washiriki 500 waliokuwa wakifuatilia kwa njia ya mtandao kutoka maeneo tofauti ya dunia.
Pia Prof.Lema amebainisha baadhi ya
mapendekezo yaliyotokana na mkutano huo kuwa ni pamoja na kuwa na chombo kitakachokuwa
kinashauri upande wa Effort(Kanda),uhitaji wa kubadili mitaala ya Elimu kuanzia
chini hadi juu ili TAIFA linufaike na mapinduzi ya Viwanda .
Prof. Lema ametaja mapendekezo mengine ni
pamoja na Kuifanya Dodoma kuwa jiji la mfano kwa kupendeza na miundombinu
iliyobora (Smart City),kuhamasisha Sera ili ziende kwenye Usajili na ziweze
kutekelezwa
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya
Wahandisi kote nchini,Mhandisi Mohammed Jaye kutoka Zanzibar
ameshukuru kwa Serikali kwa kuendelea kuimarisha mkutano kwa kila Mwaka.
0 Comments