Kaimu Kamishna wa Huduma za Urekebu Naibu Kamishna wa Magereza Julius Sang’udi (Kulia) akimkabidhi funguo za gari hilo Mkuu wa Gereza Rombo ASP Lucas Mboje (Kushoto). |
📌NA MWANDISHI WETU
DHAMIRA ya jeshi la magereza kujitegemea kiuchumi
inaendelea kutekelezwa kwa vitendo ndani ya Jeshi hilo.
Akikabidhi lori aina ya Tata jijini Dodoma kwa
uongozi wa gereza la Rombo mkoani Kilimanjaro,kwa niaba ya Kamishna wa Magereza
Kaimu Kamishna wa Huduma za Urekebu Naibu Kamishna wa Magereza Julius Sang’udi
amesema gari hilo ni sehemu ya kuhakikisha gereza hilo linajitagemea.
Naibu Kamishna Sang’udi amesema jeshi hilo limeamua
kuwezesha vifaa mbalimbali ili kuyajengea uwezo magereza nchini kujitegmea
kiuchumi.
Gari hili litakuwa chachu kubwa katika maendeleo ya Gereza la Rombo na pia kuhakikisha linatumika katika miradi mbalimbali ya kukuza uchumi.Naibu Kamishna wa Magereza Julius Sang’udi
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza Rombo,Mrakibu
Msaidizi wa Magereza(ASP) Lucas Mboje amemshukuru Kamishana Jenerali wa
Magereza Suleiman Mzee kwa kufanikisha upatikanaji wa gari.
ASP Mboje amesema gari hilo ni nyenzo muhimu katika kujenga
uchumi imara wa gereza Rombo hivyo upatikanaji wake ni hatua ni furaha kwa
watumishi wa gereza hilo.
Roli hili ni msaada mkubwa kwetu,litatusaidia katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa nyumba za watumishi,pia Gereza la Rombo limepata tenda ya kukusanya taka eneo lote la halmashuri,hivyo gari hili litasaidia kuingiza kipato kwenye gerezaLucas Mboje
Maafisa wa jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja |
0 Comments