📌NA HAMIDA RAMADHANI
JUMUIYA ya Wahandisi Tanzania
inatarajia kuadhimisha siku ya Wahandisi kwa Mara ya 17 September 3 hadi 4,
2020 tokea kuanzishwa kwake jijini Dodoma .
Aidha katika maadhimisho hayo mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi,Mhandisi, John Kijazi.
Akiongea na waandishi wa Habari Leo
jijini hapa Msajili bodi ya usajili wa Wahandisi Patrick Barozi amesema
malengo makubwa ya kuadhimisha siku ya Wahandisi ni kuiwezesha Jumuiya ya
kihandisi kuonyesha Umma nini Wahandisi wa Tanzania wanaiweza kufanya katika
kuleta maendeleo ya nchi.
Malengo kuwawezesha Umma kutambua
michango tunu inayofanywa na Wahandisi wa Tanzania katika maendeleo
ya kijani na kiuchumi nchi.
Mhandisi Barozi.
Mhandisi Barozi.
Na kuongeza kusema
kuwa"Kuwawezesha waajiri wa Wahandisi na watumiaji wa huduma
za kihandisi kutambua uwezo wa Wahandisi wazalendo na kampuni za ushauri wa
kihandisi za kizalendo" amesema
SHUGHULI ZITAKAZOFANYWA SIKU YA
WAHANDISI
Amesema katika siku hiyo shughuli
mbalimbali zitafanyika ikiwemo Kongamano la Wahandisi vijana,majadiliano ya
kitaaluma,kiapo Cha Wahandisi wataalama, Maonesho mbalimbali ya
ubunifu,teknolojia na biashara, kutoa tuzo mbalimbali kwa Wahandisi na
makampuni yalioshamiri kwenye sekta ya uhandisi na kuwatambua na kuwazawadia
Wahandisi wahitimu walioufanya vizuri zaidi katiaka mitihani yao ya mwaka wa
mwisho 2019 na 2020.
Kwa upande wake Profesa Bakari
Mwinyiwiwa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi amesema moja ya Shughuli ni
kukagua miradi na kuona kama ina kiwango au ipo chini ya kiwango.
Aidha amesema kwa muda wa miaka
mitano jumla ya Wahandisi 264 waliofanya kazi zisizo na kiwango wamechukuliwa
hatua za kisheria na watakao kula kiapo siku hiyo ni 5050.
0 Comments