📌NA HAMIDA RAMADHANI
JAMII imeshauriwa kuacha ushabiki usio na tija hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 2020 na imetakiwa kuchuja na kuangalia sera bora zinazotolewa na wagombea .
Hayo yamesemwa leo na askofu Julius Bundala Wa kanisa la Pentecostal Holliness Association Mission lilipo kata ya Makole jijini hapa wakati akifungua semina ya kina mama ya siku nne kanda ya Kati yenye lengo la kujifunza neno la Mungu,malezi ya familia, maisha ya ndoa, na ujasiriamali.
Sasa hivi kumekuwepo na ushabiki mkubwa hasa kwenye vyama vya siasa na kwenye vyama vya mipira kwa maana ushabiki wa namna hiyo utatupelekea nchi yetu kuingia katika machafuko.
Askofu Julius Bundala .
Aidha amesema kama waliweza kufunga na kuomba kwa kipindi cha janga la Corona wana imani hata mchakato wa uchaguzi wataenda kuombea taifa ili wapatikane viongozi walio Bora.
Tunatakiwa kuijiombea na kuwaombea viongozi wetu wanaokuja kutuongoza wapite Kwa amani nchi yetu ibaki na amani kwani pasipo amani hakuna maisha wananchi jiandaeni kupiga kura
Sambamba na hayo Askofu Bundala amewataka wanawake wajiamini na waache ile dhana potofu ya kusema mwanamke ni kiumbe dhaifu
0 Comments