📌NA HAMIDA RAMADHANI
JAMII imeshauriwa kuondoa mtazamo
hasi kuhusu dawa za tiba asili na badala yake imetakiwa kutumia dawa hizo kwani
ni dawa zitokanazo na mimea kwani nibora kwa matumizi ya binadamu .
Akizungumza na waandishi wa
habari katika viwanja vya Nyerere Square Mkurugenzi kutoka Khaira
Herbal Clinic Dkt. Sungura Rashid Sungura kutoka mkoani
Kigoma kwenye Maadhimisho ya siku ya tiba asili ya mwafrika amesema dawa hizo
ni dawa zitokanazo na miti iliyopo nchini na inapimwa na mkemia Mkuu kwa
matumizi sahihi ya binadamu.
Zamani hapakuwa na hospital nyingi wazee wetu walitumia dawa za asili na ndio maana kama ukifatilia utasikia kuna yale maneno huo udongo wa zamani yani na wana nguvu kabisa na waliishi kwa kutumia dawa hizi za asili
Dkt. Sungura
Aidha amesema kufuatia janga
la ugonjwa wa Corona dawa za tiba asili zimesaidia kutokomeza ugonjwa huo
hapa nchini na kumpogeza Rais Magufuli kwa kuruhusu wao kama waganga wa tiba
asili watafute dawa.
"Tunaona nchi zingine kwa sasa
wanajiuliza Corona imeishaje nchini Tanzania na niseme tu majuzi nilikutana na
gari imejaza malimao inapeleka nje ya nchi siwezi taja nchi gani karibia
magunia 200 lakini wao wanashangaa na kujiuliza Corona imeishaje nchini
Tanzania kwasababu wanataka kujaribu dawa zetu zilizosaidia kumaliza ugonjwa wa
Corona,"amesema Dkt Sungura
Mimi elimu hii ya kutibu nilifundishwa na mama mkwe wangu basi nami nikawa najiendeleza yani kama wanavyofanya mikutano wenzetu wa hospital na sisi hivyo hivyo nikawa nikikutana na waganga wenzangu tunaelekezena dawa hizi zinatibu nini.
"Nyie wenyewe mashahidi
waandishi wa Habari juzi hapa mlikuja mkaona kuna mtu anatoa shuhuda
alikua anasumbuliwa na uric acid akatumia dawa zangu kwahiyo niseme dawa hizi
zinafanya kazi vizuri na mtu anapotumia dawa hizi analeta majibu kwa
haraka na sisi huwa tunaweka mawasiliano mtu anakupigia anakupa mrejesho "
amesema Dkt Sungura
Sambamba na hayo Sungura ameishukuru
serikali kwa kuwaasa wao kama waganga watenge misitu yao kwaajili ya
kuchimba dawa ili wasiharibu uoto wa asili.
Hata hivyo maadhimisho ya siku ya
Tiba asili ya Mwafrika yalianza rasmi mwaka 2003 baada ya Mawaziri wa afya wa
nchi wanachama wa shirika la afya Duniani Kanda ya afrika kuridhia kuwepo kwa
kwa sherehe hizo.
0 Comments