Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu
wa Serikali, Bw. Doto James akizungumza wakati wa halfa ya kupokea ripoti ya tathimini
ya Mfumo wa Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato na Usimamizi wa Fedha za Umma,
ambapo amewaagiza Afisa Masuhuli wote nchini kutotengeneza mifumo yoyote bila
kupata kibali kutoka wizara hiyo, jijini Dodoma
📌NA. FARIDA
RAMADHANI NA IVONA TUMSIME, WFM, DODOMA
SERIKALI imezitaka Taasisi zote za Umma kuhakikisha zinapata kibali cha
Waziri wa Fedha na Mipango kabla ya kuanzisha mfumo wowote wa kielektroniki wa
usimamizi wa fedha za umma kama ilivyoelekezwa katika Waraka wa Hazina.
Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto
James wakati wa hafla ya kupokea ripoti ya tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki
wa Ukusanyaji wa Mapato na Usimamizi wa Fedha za Umma.
Bw. James amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango ndio yenye mamlaka ya
kutoa muongozo wa uanzishwaji wa mifumo ya usimamizi wa fedha za umma na kutoa
angalizo kuwa wote watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Nawasisitiza Maafisa Masuuli wote kuhakikisha mnapata ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mipango kabla ya kufanya ununuzi, uundaji, usimikaji na utumiaji wa mfumo wowote wa kielektroniki wa usimamizi wa fedha za umma katika mafungu au Taasisi zenu kama ilivyoelekezwa katika Waraka huoDoto James.
Amesema kuwa Serikali hufanya jitihada mbalimbali katika kuboresha na
kuanzisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki ili kuongeza
ufanisi katika ukusanyaji mapato na
kusimamia matumizi ya Fedha za Umma.
Amesema mpaka sasa Serikali imeshabuni na kutengeneza
mifumo mikubwa ya kielektroniki minne ambayo ni Mfumo
wa Ukusanyaji wa Mapato ya Kodi, Maduhuli, Tozo na Huduma Mbalimbali za
Serikali (GePG), Mfumo
wa Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi na Malipo ya Serikali (MUSE),
Mfumo wa Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo (NPMIS) na Mfumo wa Usimamizi wa
Misamaha ya Kodi.
Bw.
James amebainisha kuwa Mfumo wa MUSE unawezesha
Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri zote, Wakala
na Taasisi
zingine za Serikali kusimamia na kudhibiti mapato, malipo ya matumizi ya
kawaida na
kulipa malipo kwa njia ya kiektroniki kupitia Benki Kuu na Benki za Biashara.
Akizungumzia
Mfumo wa Usimamizi
wa Miradi ya Maendeleo (NPMIS), Katibu Mkuu huyo alisema mfumo
huo ulianzishwa
ili kuiwezesha
Serikali na
wadau wengine kupata taarifa sahihi za miradi ya maendeleo kwa wakati.
Amesema
kuwa
kila Taasisi
inayotaka kutekeleza mradi wowote wa maendeleo ni lazima ahakikishe kuwa
inatumia mfumo katika kufanya maombi na utekelezaji wa mradi. Hakuna malipo au
mgao wa pesa za maendeleo zitalipwa nje ya mfumo. Nazitaka taasisi zote zenye
miradi inayotegemea pesa kutoka Serikalini kuhakikisha miradi yote iko
kwenye kanzidata hii ya miradi”, alisema.
Katibu Mkuu huyo amesema Mfumo wa GePG
ulianzishwa kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali za ukusanyaji mapato
ikiwemo ugumu
wa kupata taarifa ya makusanyo yanayofanyika kwa wakati huo huo,
gharama
kubwa za miamala inayohusu makusanyo ya Fedha za Umma, utaratibu
usio rafiki kwa Mlipaji wa huduma za umma na machaguo
machache ya njia za kulipia (Benki, Mitandao ya simu za mkononi au Mawakala).
Amesema pia Mfumo wa
Usimamizi na Utoaji wa Misamaha ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Serikalini
umeanzishwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizokuwepo Serikalini
katika zoezi zima la usimamizi na utoaji wa misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani
Serikalini ikiwemo Wizara/Taasisi/Halmashauri kuwasilisha Wizara ya Fedha na
Mipango baadhi ya orodha za vifaa visivyokidhi vigezo vya kupata msamaha wa
VAT.
Kwa
upande wake Mtafiti aliyefanya tathmini ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanya wa
Mapato na Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Prof. Joel Mtebe, alisema kuwa, alifanya utafiti katika taasisi za
Serikali 271 kwenye mikoa 11 na kubaini kuwa mfumo umerahisisha ukusanyaji wa
maduhuri ya Serikali kwa asilimia 87 kutokana na wananchi kutokwenda moja kwa
moja katika ofisi kulipia huduma.
Naye Mhasibu
Mkuu wa Serikali, Francis Mwakapalila, alisema kuwa Mifumo ya Fedha
iliyoanzishwa na Serikali ukiwemo Mfumo wa Usimamizi na Udhibiti wa
Matumizi na Malipo ya Serikali (MUSE), umeokoa takribani Shilingi
bilioni tano zilizokuwa zikitumika kununua leseni za mifumo iliyokuwa
ikitengenezwa nje ya nchi.
0 Comments