📌NA SAIDA ISSA
MAMLAKA ya udhibiti wa maji na
nishati EWURA imeandaa muongozo wakuondoa maji taka katika makazi ya watu
ambao upo katika Sheria namba5 ya Maji na usafi wa Mazingira ya Mwaka
2019 kwa Mamlaka za maji nchini ili kuwepo na utekelezaji bora wa huduma
za Maji taka Pamoja na vyoo bora kwa wananchi.
Hayo yameelezwa Jijini hapa na
Mkurugenzi wa Mamlaka za maji EWURA Exaudi Maro wakati akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu mafunzo ya kuwajengea uwezo Mamlaka za Maji 26 ambazo
zinafanya kazi Makao makuu ya Mikoa.
Mkurugenzi huyo a kuwa ili muongozo
huo uweze kutekelezeka wameamua kuwajengea uwezo wasimamizi wa Mamlaka za Maji
nchini ambao ndio wahusika wakuu Katika utoaji wa huduma hizo.
Sasa ni jukumu la Mamlaka za Maji kuhakikisha zinatimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii kuhusu Kuwa na vyoo bora ili kuondokana na madhara yanayosababishwa na maji taka.Exaudi Maro
Alisema Sheria namba 5 imeanisha
wazi wajibu wa Mamlaka za Maji kuzalisha maji salama na yakutosha Pamoja na
Wananchi Kuwa na vyoo bora na pale inapokuwa imeshindwa kutekelezwa
wajibu wake lazima Sheria ifuate mkondo wake.
"Ndio maana tumeamua kuwajengea
uwezo Mamlaka za Maji ili Kuwa na uelewa wakutosha juu ya muongozo huu na
pale watakapokiuka ndipo hatua zitachukuliwa"alisema
Mbali na hilo amezishauri Mamlaka za
Serikali za Mitaa kwakushirikiana na Mamlaka za maji kuhakikisha zinatumia
Sheria ndogo za Serikali za Mitaa ili wananchi wawe na vyoo bora kwa lengo la
kuepekukana na magonjwa ya mlipuko.
Sambamba na hili napenda nisitize Mamlaka za maji kuwa na mfumo wa ufuatiliaji wa maji taka ili kuwa na mazingira bora katika kulinda afya za wananchi.
Exaudi Maro
0 Comments