📌NA BARNABAS KISENGI
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kilimani jijini Dodoma kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Neema Mwaluko amezindua kampeni ya uchaguzi katika
kata hiyo tayari kwa mapambano ya kutetea nafasi yake.
Awali akizungumza katika mkutano wa
uzinduzi huo uliofanyika katika mtaa wa Chinyoya Neema amesema katika miaka
mitano iliyopita katika baadhi ya maeneo katika kata hiyo kulikuwa na
changamoto kubwa mbili zikiwemo miundombinu ya barabara na urasimishaji wa viwanja vya makazi kwa wananchi wa maeneo hayo.
Ninashukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwezesha kufanikisha jambo hili pia kipekee niwashukuru mbuge Anthony Mavunde na mwenyekiti wa mtaa wa chinyoyo Faustina Bendera kwa ushirikiano wao hadi sasa tumefanikisha wananchi wetu wamerasimishiwa ardhi kwa kupimiwa.Neema Mwaluko
Aidha Neema amesema akipewa ridhaa
tena ya kuongoza miaka mitano vipaumbele
vyake ni kuhakikisha anatengeneza miundombinu ya barabara ujenzi wa shule
ya msingi ya kata,zahanati na soko ili wananchi wa kata ya kilimani wapate
huduma
Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na
mgombea ubunge wa CCM jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde amesema ili
maendeleo yakamilike katika kata ya Kilimani amewaomba wananchi wachague mafiga
matatu ya CCM,yaani Rais, Mbunge na Diwani Neema Mwaluko ili washirikiane
kuleta maendeleo.
Katika uzinduzi huo ulihudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa CCM wa Wilaya Dodoma Mjini,madiwani wateule na mbunge
viti maalumu Mariam Ditopile ambaye aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwa
wingi ifikapo October 28 mwaka huu ili wapige kura na kukipatia Chama Cha Mapinduzi
ushindi wa kishindo.
0 Comments