📌NA HAMIDA RAMADHANI
SHIRIKA la Jukwaa la Utu wa Mtoto (Children’s
Dignity Forum-CDF) linalotekeleza Mradi wa Haki ya Binti awamu ya Pili Wilayani
Mpwapwa limefanya mafunzo ya uongozi na Stadi za Maisha kwa wanafunzi wilayani
humo lengo likiwa ni kuwasaidia wanafunzi hao kutimiza malengo ambayo
wamejiwekea.
Akizungumza na CPC Blog mara baada ya kumalizika kwa
Mafunzo hayo Meneja utekelezaji wa Miradi ya CDF Bwana Evance Rwamuhuru amesema
mafunzo hayo yamelenga mambo makubwa manne ambayo ni kujitambua katika malengo
waliojiwekea ,kuwajenga katika stadi za maisha,kuwajengea uwelewa katika
masuala ya afya ya uzazi na kuwajengea uwezo katika masuala ya uogozi.
Mafunzo haya yamelenga kuwajenga wasichana pamoja na wavulana wa shule za msingi na sekondari ambao wako ishirini na mbili tumewafundisha wao kama waelimisha rika kwa maana ya kwamba wao wajifunze na waende kuwafundisha wenzao katika jamii walizotokaEvance Rwamuhuru
Wanafunzi waliopata mafunzo hayo ni kutoka shule za
Sekondari Pwaga,Kibakwe,kimagai huku kwa upande wa shule za Msingi zikiwa ni
Lupeta pamoja Ibumila.
Kupitia mafunzo haya wanaweza kujiweka malengo ya
sasa na ya baadae wanapita katika mchakato mzima wa kujua kuwa wao ni wakina
nani ,wana ndoto gani za maisha lakini changamoto gani wanaweza kukabiliana
nazo lakini sasa wanawezaje kuzikabili hizo changamoto.Evance Rwamuhuru
Amesema matarajio ya mradi huo ni kuhakikisha kwamba watoto wa kike wanafahamu haki zao na waweze kujisimamia sawa sawa kwani hawatarajii kuona watoto wa kike wanashindwa kulendelea na masomo yao kwasababu ya kupata ujauzito.
Lidya Joseph Joseph ni mwanafunzi wa shule ya
sekondari Pwaga amesemaa amejifunza namna ya kujitambua katika mafunzo hayo
kujua mwanafuni shuleni amekwenda kufanya nini .
''Nimejifunza namna ya kuweka malengo katika masomo yangu, lakini kitu kingine nimejifunza
juu ya hedhi salama, hivyo unapokuwa katika hedhi ni vitu gani msichana ufanye
unapokuwa katika hedhi ikiwemo pia kutojichafua kwani hedhi sio ugonjwa lakini
pia tumejifunza stadi za maisha hii itanisaidia sana katika masomo yangu na
hata katika maisha kwani inatusaidia namna ya kutatua matatizo ambayo yako,
nimejifunza pia namna ya kujiwekea
malengo kwa miaka mitano,kumi,kumi na tano na kuendelea'' Lidya
Wanafunzi wakijadiliana jambo katika Mafunzo ya
Uongozi na Stadi za Maisha
|
Kwa upande wa Jonh Dominick mwanafunzi wa shule ya
sekondari pwaga kidato cha tatu amesema yeye ni kwa namna gani wavulana
wanapaswa kuwasaidia watoto wa kike pindi wanapokuwa katika kipindi cha hedhi wakiwa
shuleni na sio kuwacheka.
Jumla ya wanafunzi 22 wamehudhuria katika Mafunzo ya
uongozi na Stadi za Maisha kwa wanafunzi wilayani Mpwapwa wakiwa na walimu
walezi wao 5.
Mafunzo hayo yamefanywa na Shirika la Jukwa la Utu
wa Mtoto (Children's Dignity Forum CDF) Wilayani Mpwampwa chini ya Mradi wa Haki ya Binti awamu ya Pili
kwa Ufadhili wa Comic Relief.
0 Comments