📌NA SAIDA ISSA
BENKI ya watu wa Zanzibar (PBZ) kwa
kushirikiana na Shirika la Posta Tanzania imejidhatiti kutoa huduma kwa
wahitaji na wananchi ambao wamekuwa wakienda masafa marefu kutafuta huduma.
Aidha uongozi wa Benki hiyo
umeadhimia kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma
na Seif Suleiman Mohammed meneja wa tawi la PBZ Dar es salaam pia ni msimaizi
wa mafunzo ya huduma za benki kwa mawakala wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na adhima ya benki hiyo katika kuimarisha huduma zake.
Aidha amefafanua kuwa katika
kuhakikisha huduma za kibenki zinaimarishwa kwa wananchi wote hapa nchini
wamenza kutoa mafunzo ya namna benki ya watu wa zanIbar wanavyofanya kazi.
Mafunzo haya yanatolewa hapa Dodoma kwa maafisa mbalimbali kutoka kwa mikoa tofauti ili kuweza kuboresha utoaji wa huduma za benki hiyo kwa wananchi.Seif Suleiman Mohammed
Amesema kuwa hii ni kutikana na
kwamba Dodoma ni Mkao makuu na pia ni katikati ya Nchi hivyo benki ya watu wa
zanzibar imedhamiria kutoa huduma.
Wananchi wamekuwa wakienda katika
masafa marefu ili kutafuta huduma nakuwafanya wapoteze muda mwingi na gharama.
Kwa upende wake Rehema Mbunda
meneja wa huduma za fedha na uwakala shirika la posta makao makuu Dar es
salaam alisema kuwa Benki ya watu wa Zanzibar imeamua kuingia ubia na shirika
la posta Tanzania kwa sababu tayari kwa bara kuna matawi 360 na wanatoa huduma
hivyo wananchi wengi zaidi watanufaika na ubia huo.
Wananchi watarajie kupata huduma nzuri sababu posta imetapakaa katika sehemu nyingi na sasa benki ya watu wa zanzibar imejidhatiti kuwafata wananchi mpaka vijijini ili kuwapatia huduma.Rehema Mbunda.
Amesema kuwa Benki ya watu wa
Zanzibar imeona ni bora ikatoa mafunzo kwa Maafisa kutoka mikoa tofauti
tofauti ili kuweza kutoa huduma za kibenki kwa wananchi.
0 Comments