PBZ NA TPB WAZINDUA HUDUMA ZA UWAKALA

 


📌NA.FAUSTINE GIMU GALAFONI

 

BENKI ya watu wa Zanzibari (PBZ kwa kushirikiana na   Benki ya Shirika la posta Tanzania (TPB,zimetia saini ya  makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara  na  kuzindua huduma za uwakala wa huduma za kibenki  za PBZ, kwa ajili ya  kuwahudumia wananchi.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Jijini Dodoma ,Katibu mkuu Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Mwinyi Talib Haji,amesema serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania inatambua mchango wa benki ya watu wa zanzibar hivyo ushirikiano huo utakuwa  na manufaa makubwa kwa pande zote mbili.

Aidha  amesema mwelekeo wa serikali ni kuona  mabadiliko ya dhati  katika kuiendesha  benk ya PBZ  kwa misingi ya kibiashara na kuifanya ipanuke na kuongeza wigo kwa kuwahudumia  wanancchi.

Kwa upande wao mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi PBZ,Bi  Kidawa Salehe na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Idd Makame, wameeleza kuwa  benki ya watu wa Zanzibar inamilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja kama iliovyo Shirika la Posta ndio maana imekuwa rahisi kuungana, kwani  ushirikiano huo utawawezesha kuongeza wigo wa kutoa huduma zake kwaupande wapili wa muungano  

Naye  mtendaji mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mang’ombe amesema tangu kuanzishwa kwa shirika hilo hawajawahi kuwa na mashirikiano na watu wa zanzibari hivyo wanaahidi kuwa hudumia wananchi kwa weledi ilikudumisha muungano.  

Benki ya watu wa zanzibari ilianza  kufungua matawi  Tanzania bara mwaka  2010 hadi sasa ina matawi katika mkoa wa Dar es Salam na Mtwara huku ikitarajia kufungua matawimengine  katika mikoa  7 ya Tanzania bara.

 

Post a Comment

0 Comments