📌NA
HAMIDA RAMADHANI
KATIKA kuelekea
uchaguzi mkuu nchini waandishi wa habari wameaswa kuandika na kuripoti
habari zenye haki na ukweli na kuachana na wale wagombea wanaojinadi kwa Lugha
za kejeli na matusi kwenye mikutano
Kauli hiyo imetolewa
na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kufuatia kauli ya aliyekuwa
Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa kuwahamasisha wananchi kuwasusa
waandishi wa habari na kuwataka watumie simu janja ili kupata taarifa za
habari.
Tumeona tulisemee hili mapema kwani wakianza kutoa kauli zao hizi ni hatari hasa pale mwanahabari anapokuwa kwenye majukumu yake hivyo ni lazima tulikemee kwa nguvu zetu zote ili tuwe salama kuepusha vipigo kwa waandishi wetu.Balile.
Na kuongeza kusema
kuwa "kwanza sisi hatuogopi kususiwa na kauli yake ya kusema
wametususa atambue kwqmba waandishi wa habari haitutishi bali sisi
hatutaandika habari za mgombea anaetoa lugha chafu ,matusi jukwaani
," amesema Balile
Amesema kwamba kauli
yake kwa wananchi ya kusema wawapigwe kidogo hiyo inahamasisha vurugu na
kuwachonganisha waandishi na wananchi .
Tumeona katika uchaguzi wa mwaka 2015 waandishi walipigwa Tarime sisi hatupo kwaajili ya kuandika lugha za namna hiyo isipokua chama cha siasa kijinadi kwa sera nzuri ambazo zina tija kwa jamii
Balile
Aidha amesema kuanzia
sasa mgombea yoyote ataye ripoti lugha za matusi hataripotiwa na kazi ya
mwandishi si kuripoti matusi bali ni kuangalia sera zenye tija kwa jamii kama
vile Elimu, Afya na huduma zingine muhimu kwa wananchi.
"Hivi kuna mtu
ambae yupo dunia nyingine jamani hapa wote tunapambana na hawa adui watatu
ambao ni Ujinga,maradhi na umasikini" amesema Balile
Hata hivyo amesema
nchi za nje ambazo zimeendelea, ni kutokana na wagombea wao kuwa na
Sera zenye tija na sio Sera za matusi.
VYAMA VYA SIASA.
Aidha amesema vyama
vya siasa vihakikishe vinatoa taarifa kwa vyombo vya habari kwani wana habari
si wanasiasa na kila mgombea anataka kuonekana.
Ni kweli hatuwezi kuwepo kwenye kila matukio,jambo kubwa na la muhimu wagombea watoe taarifa kwa wana habari ili habari yao iweze kurushwa tutajuaje bila kutoa taarifa?
Balile
0 Comments