📌NA HAMIDA RAMADHANI
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa
nchini (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imewafikisha
mahakamani watu watano (5) kwa makosa ya uhujumu uchumi ikiwemo makosa ya
matumizi mabaya ya fedha na kuisababishia Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa
hasara ya zaidi ya shilingi mil.149.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa
Takukuru mkoani hapa Sosthenes Kibwengo amesema makosa hayo ni kinyume na
kifungu cha sheria namba 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Amesema kuwa watuhumiwa hao ambao walikuwa ni
watumishi wa halmashauri hiyo ni Fanuel Senge( 67),aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji, Ignace Chacha(48),aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, pamoja na
Joel Nskela,aliyekuwa Afisa Mipango.
Amesema kuwa watumishi hao ambao wameshitakiwa
kwa matumizi mabaya ya mamlaka wameunganishwa katika shtaka la pili la
kusababisha hasara na Moses Ryakitimbo(38) ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya magoma and Rykitimbo Contractors LTD,na Gerald Massawe (43)aliyekuwa
Meneja mradi wa Ujenzi wa Ukumbi wa kibiashara wa wilaya ya Mpwapwa.
Uchunguzi wa Takukuru unaonyesha kuwa watu hao septemba 12 na Desemba 2013,watumishi hao walitoa zabuni ya ujenzi wa ukumbi wa biashara yenye thamani ya sh mil 356 kwa kampuni ya Magoma and Ryakitimbo Contractor LTD bila kufuata taratibu za manunuzi ya umma kwa bodi ya zabuni.Sosthenes Kibwengo
.
Kibwengo amesema uchunguzi umeonyesha
Mkandarasi alilipwa jumla ya sh milion 149,833,500.
Mbali na hilo pia wamewapandisha kizimbani
aliyekuwa Afisa Elimu Msingi Abubakary Adam (57) na aliyekuwa Afisa Elimu
Ufundi wote wa halmashauri ya Chamwino kwa kosa la kutumia nyaraka kumdanganya
muajiri kinyume na sheria.
“Watu hao wamefunguliwa mashtaka 8 ya kugushi
na shtaka moja la ubadhilifu kinyume na kifungu cha sheria namba 28.
Alisema uchunguzi wa Takukuru unaonyesha
Agosti na Oktoba 2015 watuhumiwa waligushi nyaraka mbalimbali na kujipatia
kinyume na taratibu sh milion 3.5 ambazo walidai walizitumia kutengeneza kasiki
katika shule 12 zilizopo katika halmashauri hiyo”amesema .
Kesi hiyo itatajwa tena septemba 24 mwaka huu katika Mahakama ya hakimu mkazi Mpwapwa chini ya hakimu Nuru Nasari.
Hata hivyo Mkuu huyo wa TAKUKURU amewakumbusha
watumishi wa umma kuacha kujisahau na kuwataka kufanya kazi kwa weledi.
Pia amesema kuwa watumishi wanapaswa kuwa
makini katika utendaji wao wa kazi za kila siku.
Amesema Takukuru inawakumbusha watumishi wa
umma kwamba jinai haifi unaweza kutenda kosa leo likaja kujulikana hapo
baadae.
Inawezekana ukawa hukumbuki lakini uchunguzi ukifanyika unafikishwa mahakamani bila kujua,hivyo Takukuru ipo kila kona kuangalia walarushwa hivyo jamii inapasa kuwa makini katika kazi wanazofanya.
0 Comments